KUFIKA KWA WAARABU, BIASHARA YA UTUMWA NA UISLAMU

By , in MAENDELEO YA KISWAHILI on . Tagged width:
WAARABU
Waarabu walifika katika pwani ya Afrika ya Mashariki zamani sana; hata haijulikani ni lini walifika Tanganyika kwa mara ya kwanza. Warabu walikuja Tanganyika kufaanya biashara ya dhahabu, watumwa, pembe za ndovu, za vifaru na magamba ya kobe. Tangu zamani sana, nchi za Afrika Mashariki zilijulikana na watu wa Mashariki ya Kati. Inasemekana kuwa Waarabu walifika hapa Afrika Mashariki kabla ya kuzaliwa Kristo (KK).
Waarabu walifika Tanganyika, kwa sababu kuu mbili. Kwanza, Waarabu wako karibu na Afrika Mashariki. Pili, majahazi yao yalikuwa yanasukumwa na upepo badala ya mashine. Kuja na kurudi yalisukumwa na pepo za Monsoon. Pepo hizi za Monsoon, katika mwaka, msimu mmoja, huvuma kutoka Kaskazini Mashariki, na katika musimu wa pili hugeuka na kuvuma kutoka Kusini Magharibi. Kwa hiyo zilipovuma kutoka Kaskazini Mashariki ziliwaleta Waarabu katika pwani ya Afrika Mashariki na zilipogeuza katika musimu wa pili, na kuvuma kutoka Kusini Magharibi ziliwarudisha Mashariki ya Kati. Hata hivyo si wote waliorudi kwao. wengine walibaki hapa pwani ya Tanaganyika; wakaoana na Waafrika wa pwani. Uzao wao wakaitwa Waswahili. Swahili kwa Kiarabu ni pwani. Lugha yao ni Kiswahili. Kiswahili ni lugha ya Kibantu yenye maneno mengi ya Kiarabu. Na kipindi kirefu Kiswahili kimekuwa kiungo cha makabila ya Tanzania na wageni kutoka nje. Walipokuja hapa walijifunza Kiswahili.
Historia ya Misri inasema kuwa Wamisri walikuwa wanafanya biashara na nchi za kusini mwa bahari ya Shamu. Walifika mpaka Punt; ambayo, sasa ni Elitria na Somaliland. Safari ya kwanza iliyoandikwa ilikuwa mwaka 2500 BC. Zamani kabla ya Ibrahimu. Safari zao nyingi, walienda kusini na kuleta miti ya mafuta ya manemane; ilikuwa wakati wa kipindi cha wa Israeli walipokuwa watumwa huko Misri. Taarifa ya safari hii imepatikana katika chumba cha maiti, cha Malkia, Hatshop Sut, huko Misri.
Pia kuna taarifa kuwa Mfalme Suleiman; Mfalme wa Waisrael. Mfalme aliyekuwa tajiri sana kupita matajiri wote wa wakati huo. Aliunda kikosi cha merikebu za biashara, katika pwani ya Bahari ya Shamu. Mfalme wa Edomu, Hiramu, alimpa Mfalme Suleiman mabaharia wake waliokuwa wadhowefu wa bahari; waende pamoja na mabaharia wa Mfalme Suleiman. Walienda kusini mpaka wakafika Ophir. Wakamletea Mfalme Suleiman, dhahabu yenye uzito wa talanta 420; (talanta 1=ratili 150).
Kabla ya karne ya 10 Baada ya Kristo (BK); waandishi wa Kiarabu waliandika juu ya mlolongo wa serikali za miji (city states) ya Kiarabu katika pwani ya Afrika Mashariki. Miji hii ilikuwa huru, yenye serikali zinazo tawaliwa na koo za Kislutan. Hakukua na serikali moja iliyotawala pwani ya Tanganyika. Hata hivyo, mji wa Kilwa katika pwani ya kusini mwa Tanganyika, kwa kipindi kirefu ndio ulikuwa kitovu cha biashara; na kutawala njia kuu za misafara ya biashara ya dhahabu kutoka kusini.
Mfanya biashara Ibin Batuta kutoka Uarabuni, alitembelea miji hii mwaka 1331. Anaelezea uzuri wa misikiti aliyoiona katika miji hii na wajihi au haiba (personalty) ya masultani wa miji hii. Alipendezwa sana na lugha ya Kiswahili na utamaduni wa Waswahili na ukarimu wao. Wasafiri wote waliotembelea miji hii ya Kiarabu katika pwani ya Tanganyika hawataji chochote kuhusu elimu ya wakazi wa miji hii. Hawasemi hali ya shule na vyuo walivyo viona. Bali wanasifu uzuri wa misikiti, maendeleo ya biashara ya kimataifa iliyokuwa inafanywa kati miji ya pwani na nchi za nje. Ushahidi uko mpaka leo, vigae vya sahani bakuri, na mabaki ya vitu vingine kutoka nchi za mbali bado yanaonekana. Mabaki mengine ambayo bado yanaonekana mpaka leo ni ya nyumba za Warabu, ngome zao na makaburi yao. Mambo ambayo hakuyaona ni majengo ya shule, vyuo na hospitali. Ni dhahiri kuwa vitu hivi havikuweko. Kuhusu matibabu, inaelekea kuwa Warubu walitibiwa na dawa zao za Kiarabu. Waafrika hali kadharika, walitibiwa na waganga wa kienyeji kwa mitishamba.
Kilwa ndio mji uliokuwa kitovu cha biashara, kati ya Afrika Mashariki na nchi za nje za Arabia, Uajemi (Persia), India, China. Lakini hakukua na uhusiano wa kibiashara na makabila ya bara ya Tanganyika. Mji huu wa Kilwa baadaye ulipata changamoto kutoka miji mingine ya pwani ya Afrika mashariki. Zaidi ilikuwa ni Zanzibar na Mombasa. Miji iliyokuwa inapiga hatua kubwa za maendeleo ya biashara.
Mwanzoni mwa miaka ya 1700, Baada ya Kristo, Sultani wa nchi ya Kiarabu, ya Oman, aliteka Pemba na Kilwa.Na badae miji yote ya Pwani ya Afrika ya mashariki ikawa chini ya utawala wa Sultaani wa Oman. Mwaka wa 1840, Said bin Sultani alihamisha makao makuu ya himaya yake, kutoka Oman, akahamia Zanzibar. Sasa pwani yote ya Afrika Mashariki na Oman Uarabuni, ilikuwa chini ya serikali ya Zanzibar. Utajiri wa Zanzibar ulitokana na mashamba ya Karafuu na minazi, sehemu nyingine ilitokana na biashara ya Watumwa na pembe za ndovu. Watumwa na pembe za ndovu zilisafirishwa kutoka Magharibi mwa Tanganyika mpaka Bagamoyo. Kufikia mwaka wa 1850 biashara ya watumwa napembe za ndovu ilifika mpaka Kongo.
Kwa kifupi, Waarabu walikuwepo katika pwani ya Afrika mashariki tangu zamani sana. Walizoea kuingia na kutoka; na wengine wakahamia kabisa. Walisadia kuijenga lugha ya Kiswahili ambayo sasa ndiyo lugha ya Afrika Mashariki. Ingawaje biashara yao ya utumwa na ukatili wao uliopindukia umeacha makovu yasiyo futika.
BIASHARA YA WATUMWA
Kwa kipindi kirefu ambacho hakijulikani mwanzo wake; Warabu waliendesha biashara haramu, Tanganyika. Walishambulia vijiji vya Waafrika na kuteka watu na kuwafanya watumwa; ambao waliwauza Uarabuni, Zanzibar na nchi nyingine za nje. Kwa Zanzibar walitumika katika mashamba ya Karafuu na minazi. Lakini wengi walisafiriswa mbali na pwani ya Tanganyika. Walionunuliwa na Wazungu walipelekwa Amerika. Lakini Wazungu hawakununua watumwa wengi kutoka Afrika Mashariki. Wazungu walinunua watumwa wengi kutoka Afrika ya Magharibi.
Waarabu waliokuwa wanafanyabiashara ya utumwa walikuwa katili kupindukia. Watumwa walipitia katika mateso yasiyo kifani. Walitendewa, ukatili wa kinyama, usio wa kiutu wala ubinadamu. Watumwa, walipigwa, waliuawa. Walifungwa mikatale. Walitembea kwa miguu mwendo mrefu wakiwa wamefungwa minyororo miguuni au shingoni; huku wakibeba meno ya tembo na mizigo mingine na walikipigwa kwa kutembea polepole. Walitembea kwa miguu toka Ujiji, Kigoma mpaka Bagamoyo. Wagonjwa na dhaifu waliachwa mapolini wafe peke yao au waliwe na wanyama.
Historia inasema kuwa wakati wa miaka ya 700 Kabla ya kuzaliwa Kristo (700KK); katika nchi ya Irak, kulikuwa na watumwa wa Kiafrika, wengi kiasi chakutosha kufanya uasi wa kutaka kupindua nchi. Kwa kipindi cha miaka 200 uasi huo uliokuwa unatokea mara kwa mara ukianzishwa na watumwa wa Kiafrka. Hii ina maana kuwa Waafrika walikuwa wakitekwa na kuuzwa kama watumwa huko Mashariki ya kati kwa kipindi kirefu.
Biashara ya watumwa ilikuwa mbaya sana baada ya maendeleo ya silaha hasa, bunduki. Waarabu waliwapa bunduki Waafrika waliowasaidia katika biashara hii. Waliopewa silaha, waliikuwa wanashambulia Waafrika wenzao na kuwateka; halafu kuwauza kwa Warabu. Waliteka wanaume na wanawake; wengi wao wakiwa wavulana na wasichana. Pia machifu nao walishambulia vijiji vya jirani na kuteka watu halafu waliwauza kwa Warabu. Wakati mwingine walikamata raia wao wenyewe na kuwauza kwa Warabu.
Msafara mmoja wa watumwa ulikuwa na watuma zaidi ya 1000. Lakini si wote waliofika pwani, pengine walifika 1/5; wengi wao walikufa njiani kwa ajili ya mateso magonjwa na waliochoka na kuwa dhaifu, walitekelezwa mapolini bila msaada wowote. Walioachwa ilikuwa vigumu kurudi kwao walikotokak, wa ajili ya umbali, udhaifu, kutokujua njia na hatari za wanyama wakali, njaa na kiu.
Haijulikani idadi kamili ya watumwa waliokuwa wanafika Bagamoyo. Inakadiliwa kuwa walikuwa zaidi ya 50,000 kwa mwaka. Watumwa walipofika Bagamoyo, walibwaga mioyo yao, ‘Bwagamoyo’ yaani walikata tama. Walijua kabisa, wakisha ingizwa kwenye majahazi ya Waarabu, milele, hawatarudi kwao. Biaashara ya Watum, ilikuwa mbaya sana katika karne ya 19. Watumwa waliacha ndugu, jamaa, mali zao na nchi yao na kupelekwa mbali na kwao; na kuishi maisha ya kutumikia mabwana zao; ujila wao kupigwa na kuteswa. Waliishi maisha yasiyo na matumaini. Waliojaribu kutoroka, walipopatikana waliuawa mbele ya wenzao, ili iwe fundisho kwa wengine.
Mwaka wa 1847, manowari ya kivita ya Kiingereza, katika Ghuba ya Uajemi, iliokoa watumwa wa kwanza kuokolewa kutoka jahazi la Warabu. Watumwa waliookolewa walikuwa wasichana 43 na wavulana 12. Watumwa waliookolewa walipelekwa India, Bombay. Sir Bartle Frere, Gavana wa India alifurahishwa sana na kitendo cha kuokolewa kwa hawa vijana. Kwa hiyo alitoa pesa za serikali kuwasomeshea vijana hawa. Vijana 200 kati ya vijana watumwa waliokuwa wanaokolewa kutoka majahazi ya Warabu wakienda kuuzwa, walisomeshwa India. Mwaka 1864, kati ya vijana 3 walosoma India walipelekwa Rabai, Kenya. Wawili kati yao walikuwa mapasta wa kwanza wa Waafrika wa kanisa la Kianglikana, Kenya.
Mwaka 1862 Father Horner wa Roman Katoliki alianzaisha makazi ya Watumwa waliokuwa wanakombolewa katika majahazi ya Warabu huko Zanzibar. Mwaka uliofuata alianzisha makazi mengine ya watumwa waliokombolewa huko Bagamoyo. Watumwa waliokombolewa na walioonyesha uwezo mzuri walifundishwa masomo ya kawaida; wengine walifundishwa kilimo, ujenzi na ufundi wa aina mbalimbali, ili waweze kujitegemea.
Sultani wa Zanzibar alipendezwa na matokeo ya kuwatunza watumwa waliokombolewa. Mwaka 1869 alitoa ardhi kubwa akawapa Wamishonari waitumie kwa kilimo cha mashamba ya Watumwa walio kombolewa. Makazi ya watumwa waliokombolewa yaliwawezesha watumwa waanze maisha mapya ya kujitegemea na kusahau mateso ya Utumwa.
Katika mwaka wa 1864 wa Misionari wa UMCA walikuja pia. Nao walianza kazi ya kuwahudumia Watumwa waliokombolewa. Mpaka mwaka 1873 Wamishonari wa UMCA walikuwa wanatunza watumwa waliokombolewa 110. Wanakuwa na watu wengi sana. Malengo yao yalikuwa kuwaelemisha ili wawe watumishi wa kanisa; walimu, wainjilisti na makasisi. Walitazamia baadae wawasaidie katika huduma ya kupeleka Injili kwa watu. Huko Zanzibar walinunua ardhi mahali panapoitwa Mbweni ili yawe makazi ya Watumwa waliokombolewa.
Mwaka 1888, Kadinari Lavigeria, kiongozi wa shirika la Romani Katoliki la White Fathers alisema kuwa Afrika ilikuwa inapoteza watu 400,000 kwa mwaka waliokuwa wanakamatwa na kwenda kuuzwa na kuwa watumwa. Biashara hii iliwafanya Waafrika wachanganyikiwe na kukosa amani na mwelekeo wa maisha. Hawakuweza kufanya maendeleo yoyote. Daima walikuwa wanakimbia na kujificha, wakiogopa kukamatwa na kufanywa watumwa.
Dkt. David Livingstone, miaka yake ya mwisho ya maisha yake aliitumia katika Afrika ya Mashariki. Makazi yake yakiwa Ujiji, Kigoma. Ujiji ndiyo ilikuwa kitovu cha Biashara ya Utumwa. Maelezo yake kuhusu Biashara ya Utumwa iliwasitua Wazungu Ulaya, hasa Waingereza. Anaeleza kuwa aliona vijiji vilivyobomolewa na kuchomwa moto, mashamba yaliyochomwa moto. Mifupa ya watu waliokufa ya zamani na mipya. Mifupa ya watu waliokufa ilitapakaa kwa umbali wa maili nyingi. Dkt. Livingstone aliendelea kuwasisitizia Wazungu wa Ulaya madhara ya Biashara ya Utumwa.
Baadhi ya Wamishonari wa Kijerumani walitafuta wakoloni wa Kizungu kuja kutawala Afrika ya Mashariki ili kukomesha Biashara ya Watumwa. Na kuwaacha huru Wafrika waendeleze uchumi wao. Dr. Livingstone pia alisisitiza sana kutafuta Wakoloni wa Kizungu kuja kutawala Afrikana kuokoa Waafrika kutoka Biashara ya Watumwa iliyokuwa ikiendeshwa na Warabu. Wamishonari wa Kanisa la Methodist pia nao walikuwa wanatafuta Wakoloni waje kutawala na kuokoa Waafrika.
Krapf Mjerumani, mgunduzi; alirudi Ulaya mwaka 1850 baada ya kuwepo Afrika kwa kipindi cha miaka 13. Alitoa taarifa kuhusu Utumwa katika pwani ya Afrika Mashariki. Kabla ya kurudi Ulaya alifanya safari ya jahazi kutoka Tanga mapaka Msumbiji na kurudi. Alijionea mwenyewe uharibifu na uharifu uliokuwa unafanywa na Warabu kutokana na Biashara ya Watumwa. Krapf alilipoti madhara ya Biashara ya Utumwa Ulaya kabla ya Dkt, Livingstone.
Sultan Seyyid Said, Sultani wa kwanza wa Zanzibar, kuanzia mwaka 1806 – 1856. Alifanya mkataba na Waingereza kupunguza Biashara ya Watumwa. Sultani Barghash, Sultan wa tatu wa Zanzibar kuanzia 1870 – 1888, mwaka wa 1873 alilazimishwa na serikali ya Uingereza kukomesha Biashara ya Watumwa katika Afrika Mashariki. Na alifanya hivyo. Mwaka 1876 – 1877 Biashara ya Utumwa ilikomeshwa. Lakini usafirishaji wa watumwa kwenda Zanzibar na Uarabuni ulifanywa kwa siri. Vijiji viliendelea kushambuliwa walioshambuliwa walifanywa mateka mpaka watoe meno ya tembo ndipo waachiwe huru.
IBEA (Imperial British East Africa Co.) Hii ilikuwa ni kambuni ya Kiingereza iliyokuwa inawakilisha Waingereza Afrika ya Mashariki. Mwaka 1887, Kambuni hii ilitiliana sahihi na Sultani Barghash, Sultani wa Zanzibar, ili akomeshe biashara ya Utumwa Afrika Mashariki. Kambuni ya IBEA ilianza kufanya kazi ya kukomboa watumwa na kuwaacha huru mwaka 1888. Viongozi wa kampuni hii walikuwa William Mackinnon na Buxton. Katika kipindi cha miaka 3 IBEA iliwaacha huru watuma 4000. IBEA ilikuwa inanunua watumwa na kuwaacha huru. IBEA Ilinunua watumwa hao 4000 kwa mabwana zao kwa paundi za Kiingereza 3,500. Kambumi ya IBEA na Wamishanari walikuwa wananunua watumwa kutoka kwa mabwana zao. Kila walipopata habari kuwa kulikuwa na Waarabu waliotaka kuuza watumwa wao, basi waliwahi kuwanunua kabla ya kununuliwa na wengine ambao wangaliendelea kuwafanya watumwa.
Wakati mwingine, watumwa walitoroka na kujisalimisha kwa wamishonari au kwenye kambuni hii ya Kiingereza. Wamishonari hawakuwarudisha kwa mabwana zao; bali waliwaacha huru na kuwatunza pamoja na kuwalinda. Kitendo cha kutowarudisha watumwa kwa mabwana zao kilikuwa kinawakasirisha sana Waarabu. Wamishanari walianzisha miji huru, (Free towns). Miji waliyokuwa wanawaweka watumwa waliokombolewa. Waliwatunza na kuwalinda pamoja na kuwafundisha kilimo na ufundi mbalimbali.
KUFIKA KWA UISLAMU TANGANYIKA
Uislamu ulianzia Mashariki ya Kati katika karne ya saba. Baada ya kuzaliwa Kristo (BK); na ulifika katika pwani ya Afrika Mashariki katika karne hiyo hiyo. Uliletwa na Warabu wafanya biashara ya Utumwa na meno ya tembo; waliokuwa wanakuja na kutoka. Kwanza ulipokelewa na Warabu na Machotara waliokuwa wanaishi katika pwani ya Afrika Mashariki. Warabu, ndilo taifa la kwanza lililoendelea kufika na kukaa Tanganyika na Uislamu ndiyo dini ya kwanza ya kigeni kuja Tanganyika. Waafrika wawakati huo walijua kuwa ustarabu na maendeleo ni kuwa kama Mwarabu. Kufuata utamaduni wa Kiarabu, Kuingia dini ya Kiarabu, yaani kuwa Mwislamu na kufanya biashara kama Mwarabu.
Uislamu uliingia Tanganyika kwa njia tofauti na ulivyoingia na kuenea Mashariki ya Kati na Afrika ya Kaskazini. Mashariki ya Kati na Afrika ya Kaskazini Uislamu uliingia kwa njia ya vita vya Jihad. Kabla ya Mtume Muhamadi kufariki, waislamu walipigana, wakiongozwa na Mtume mwenyewe, kama vile vita ya Badr, vita ya Uhud, vita vya Khndak, vita vya Bian-Al-Muswt walik, vita vya Khaybar, vita vya Hunayn, vita vya Taif, vita vya Tabuk, na hata baada ya Mtume kufariki Waislamu waliendeleza vita hivi, vya Jihadi na kuteka nchi. Kila nchi iliyotekwa, watu wake walisilimu na kuwa Waislamu
Kabla ya karne ya saba, nchi zote za Mashariki ya Kati na Afrika ya Kaskazini, na Mashariki, watu wake walikuwa Wakristo, zilikuwa nchi za Kikristo, kwa kuwa Ukristo ulianzia Palestine. Vita hizo zilifuta kabisa Ukristo katika maeneo hayo. Ukristo ulirudi baadaye kufuatilia juhudi za Wamishonari kutoka ulaya.
Hapa Tanganyika, mambo yalikuwa tofauti. Waafrika wengi wa pwani na waliokuwa katika njia kuu ya kusafirishia watumwa kutoka bara mpaka Bagamoyo na katika vituo vya biashara kwa hiari yao wenyewe na bila kushurutishwa na mtu yeyote, walisilimu. Kwa hiyo, Uislamu uliingia kwa amani, hakuna vita yeyote, iliyopiganwa kati ya Waislamu na Watanganyika.
Waarabu hawakuwa na nia ya kueneza Uislamu katika makabila ya Bara Sababu kubwa zilikuwa, Waarabu walioendesha biashara ya watumwa walikuwa Waislamu. Na dini ya Kiislamu inakataza Mwislamu kumfanya Mwislamu mwingine kuwa mtumwa wake. Kama Watanzania wengi wangeingia Uislamu, Waarabu wangalikosa maeneo ya kuteka watumwa.
Wakati wa Waarabu wanatawala hapa Tanganyika, makabila ya bara yalibaki na dini zao za jadi. Makabila yaliyoingia Uislamu ni yale tu yaliyoshirikiana na kufungamana na Waarabu katika biashara ya Watumwa. Waafrika walishawishika kuingia Uislamu ili wajiepushe na kukamatwa na kufanywa watumwa. Pili, Waafrika wenzao waliosilimu walionekana kama walioendelea, wastarabu na walishirikiana na Waarabu kwa ukaribu zaidi. Hali hii, iliwavutia Wafrika wengi, wapende kuigia dini ya kiislamu. Kwa Mwafrika maendeleo ni kuwa kama Mwarabu.
Serikali ya Kijerumani ilisaidia kueneza Uislamu bara. Wajerumani walitumia Waswahili, Waislamu, kwa kazi zao na zaserikali. Waislamu walikuwa wastarabu tena ndio pekee waliokuwa na elimu ya awali; waliojifunza kwenye madrassa. Walijuwa kusoma na kuandika herufi za Kiarabu. Walizungumza Kiswali, lugha iliyoeleweka na wengi. Kwa hiyo watumishi wa serikali walikuwa Waislamu. Wajerumani walipokuwa wanasafiri ndani ya nchi, walifuatana na Waislamu. Hata Wamishonari walitumia Waswahili waliposafiri. Kwa njia hii walisaidia kueneza Uislamu.
Zaidi ya serikali ya Kijerumani kuwatumia Waswahili katika kazi za serikali, pia waliwasomesha. Wajerumani walisaidia katika kuwaelemisha Waislamu. Wakati huo Waislamu walikuwa mbele ya Wakristo kielimu. Wakati, Wamishonari walipofika Tanganyika, katika karne ya kumi natisa, walikuta, Wajerumani wakiwaelemisha Waislamu; ndipo na wao wakaomba serkili isaidie kuwaelemishia Wakristo waliokuwa Bara. Pia waliiomba serikali kuwa, Wakristo nao waajiriwe serikalini kama wenzao Waislamu. Kwanza serikali ilisita kuwasaidia Wakristo, lakini baadae walianza kutoa misada kusaidia elimu ya Wakristo pia, kama ilivyofanya kwa Waislamu.
Kuongezeka kwa idadi ya Waislamu, na kuendelea kielimu kuwazidi Wakristo, ilikuwa changamoto kwa Wamishonari. Ili kuweza kukabili changamoto la kutokuajiriwa Wakristo selikalini, Wamishonari walihakikisha kuwa Wakristo wanapata elimu bora kuwapita Waislamu. Kwa hiyo hatua iliyofuata ni makanisa kufungua shule nyingi za kuwaelimishia Wakristo. Kanisa la Romani lilikuwa mbele katika kufungua shule nyingi inchini. Madhehebu mengine pia yalifungua shule zao. Shula za kanisa zilitoa elimu bora kupita ile iliyokuwa inatolew na serikali. Matokeo yake Wakristo waliosoma waliongezeka na kuwazidi Waislamu waliongojea kusomeshwa na serikali peke yake. Wakristo sasa walisomeshwa na serikali na pia na makanisa yao. Hapa ndipo kwa mara ya kwanza Wakristo wana wazidi elimu Waislamu; mpaka leo. (Soma The Missionaries Factor in East Afrca. E Oliver. Uk 202 – 207). `Kwa maika yote ya Warabu kukaa hapa Tanganyika hawakujishughulisha na kueneza dini ya Kiislamu kama walivyofanya Mashariki ya Kati na Afrika ya Kaskazini. Wala kuelemisha Waafrika.
Kwa Mwislamu mtu ambaye si mwislamu ni kafiri na kafiri hana thamani mbele za Mwislamu na Mungu. Hata kuuwa kafri hakuna dhambi ila aliyeua kafiri anapata dhawabu kutoka kwa Mungu. Kwa hiyo kuna baadhi ya Waafrika waliogundua hilo; na walijikinga na kufanywa watumwa kwa kusilimu. Mwafrika aliyesilimu hawezi kufanywa mtumwa; hofu ya kumwogopa Mwarabu inaondoka na atashirikiana na Warabu kwa karibu sana. Atajifunza kusoma na kuandi ka Kiarabu na kusoma Kurani. Kwa bahati mbayaWatanzania waliojua siri hii ni Waafrika wa Pwani. Huko bara hawakujua kinga hii; kwa hiyo waliendelea kukamatwa na kufnywa watumwa.
Kama Waarabu wangaliamua kufanya jitihada ya kueneza Uislamu, Tanganyika, Watanganyika wengi wangelisilimu. Na Warabu wangalikosa eneo la kuteka watumwa. Biashara ya watumwa kwa Tanganyika ingaliishia karne ya saba kwa kuwa Uislamu ulifika hapa mapema katika karne hiyo hiyo, ulipoanzishwa huko Mashariki ya kati. Lakini Waarabu hawakutaka kuwasilimisha Watanganyika ili waendelee kuwa na eneo la kukamata watumwa.
Kwa kipindi chote Warabu walichokaa hapa, wangaliwasilimisha Watanganyika, leo hii, Tanganyika ingalikuwa nchi ya Kiislamu kama huko Libiya, Tunisi na nchi nyingine za Afrika ya Kaskazini. Wala kusingalikuwa na Tatizo la kujua ni nani wengi kati ya Wakristo na Waislamu. Kwa kuwa dini ingalikuwa moja, na karibu kila mtu angalikuwa Mwislamu. Utamaduni, mila na desturi, ingalikuwa za Kiislamu. Tatizo la Mahakama ya Kazi na OIC lisingalikuweko. Kwa hiyo, Waislamu kuachwa nyuma kielimu na maendeleo hayakusababishwa na Mjerumani, Mwingereza, Mwalimu Julius Nyerere wala Mfumo Kristo. Mchawi anafahamika lakini kwa makusudi anafichwa. Baada ya Waingereza kukomesha biashara ya utumwa, Warabu waliishi na Waafrika kwa amani. Uislamu ukawa alama ya ustaarabu badala ya utumwa na mateso.
Wakoloni wa Kijerumani na Wakristo waliingia hapa Tanzania katika krne ya kumi na tisa. Walikuta Uislamu ukiwepo hapa tangu karne ya saba; yaani Uislamu ulikuwepo hapa kwa kipindi cha zaidi ya karne kumi na mbili; miaka zaidi ya 1200. Kwa kipindi chote hicho Uislam kwa Waafrika ulibaki kwa makabila ya Pwani tu. Kama Warabu wangekuwa na nia ya dhati kueneza Uislamu hapa Tanganyika, Wajerumani wangekuta karibu watu wote ni Waislamu.
Katika miaka hiyo 1200 Waislamu, au Waarabu hawakujenga chuo wala shule hata moja. Bali, walijenga misikiti, iliyotumika kwa ibada na kwa kuwafundisha waumini wao elimu ya awali; kusoma kuandika na hesabu nyepesi na waliandika kwa kutumia herufi za Kiarabu. kukariri kurani na mafundisho mengine ya dini ya Kiislamu. Hawakujenga shule za kawaida, wala hospitali. Waliwafundisha waumini wao wa kiafrika kuswali, kusoma na kuandika Kiarabu. Kulikuwa hakuna shule zenye mfumo wa shule zenye viwango kama shule za msingi, sekondari na vyuo vikuu, kama vilivyo azishwa na Wazungu. Shule ya kwanza hapa Tanganyika ilijengwa wakati wa ukoloni wa Kijerumani. Ilijengwa huko Bagamoyo. Jengo la shule hii liko huko Bagamoyo mpaka hivi leo. Kama Waarabu wangalijenga shule na vyuo, Uislamu ungalikuta Waafrika wameshaendelea. Kama nchi za Ulaya, za Mashariki ya kati zilivyo endelea. Wazungu pia waliokuja katika karne ya kumi na tisa, wangalitukuta tumeendelea. Wasingeliita bara letu kuwa ni bara la giza. Kwa kuwa wangelikuta maprofesa, madakitari na wataalamu mbalimbali. Lakini Wazungu, walitukuta tukiwa katika giza totolo. Walikuta waislamu wakiwa na elimu ya awali ya kujua kusoma na kuandika herufi za Kiarabu. Wakoloni wa kizungu walikaa hapa kwa kipindi kama cha miaka sitini tu, tukaweza kujitawala wenyewe na tulikuwa na kisomo cha juu. Tulikuwa na madaktari wa elimu mbalimbali.
Kwa kuwa Waarabu walikuwepo hapa kwa kipindi cha karne nyingi kabla ya Uislamu. Uislamu ungaliwakuta Watanzania wakiwa wamendelea kiasi cha kutosha. Hata hii tunayosema elimu ya awali ilisomeshwa na Waislamu, kwa kuwa walitaka Waislamu wasome Kurani. Lakini kabla ya Uislamu Waarabu walishughulika na biashara tu. Kisomo na maendeleo yalikuweko huko Mashariki ya kati kwa karne nyingi sana. Hata kabla ya kipindi cha Musa watu wa Mashariki ya Kati walikua wameishaelimika na kuwa na utaalamu mbalimbali. Waligundua dawa za kuhifadhi maiti kwa kipindi cha miaka mamia kama si maelfu. Walijenga majengo makubwa na ya ajabu mpaka leo hii, kama mapiramidi ya Misri na kadhalika
ALIYEDIDIMIZA ELIMU NA MAENDELEO YA WAISLAMU?
Ni nani aliyedidimiza elimu na maendeleo ya Waislamu? Je, ni wakoloni wa Kizungu, Wajerumani na Waingreza? Rais wa kwanza wa Tanganyika, Mwalimu Julius Nyerere? Au Mfumo Kristo, Kama inavyodaiwa na Waislamu? Madai haya yote si ya kweli. Wazungu hawakuwa wakoloni wa kwanza walio tawala Tanganyika. Mkoloni wa kwanza alikuwa Mwarabu ingawa baadae aliingiliwa kati na Mreno, lakini baadae Mreno aliondoka akamwachia tena Mwarabu; akiendelea kutawala Tanganyika, kwa kipindi cha Karne nyingi; kabla ya Wajerumani na Waingereza na hata Mwalimu Nyerere kutawala Tanganyika.
Wakristo walikuja Tanzania miaka 40 kabla ya ukoloni wa Kizungu. Wajerumani walianza kutawala Tanganyika mwaka 1884/85. Kwa hiyo Wakristo walifika Tanzania mnamo mwaka 1844/45. Hii ni karne ya 19 na Uislamu ulifika hapa mnamo karne ya 7. Kwa hiyo kipindi cha kati ya kufika Uislamu na Ukristo ni karne 12 yaani miaka kama 1200.
Wakristo na Wakoloni wa Kizungu walipofika Tanganyika kwa mara ya kwanza hawakukuta Waafrika, Waislamu waliosoma au wenye elimu. Waislamu wengi walikuwa wmesoma elimu ya awali. Walijua kusoma, kuandika herufi za Kiarabu na hesabu kidogo. Hakukua na chuo wala shule za kati (sekondari) hata moja. Masomo ya awali walisomea misikitini. Ushahidi ni kwamba hatuoni magofu ya vyuo, shule, hospitali hata moja. Tunachoona ni magofu ya misikiti. Makazi yao, ngome zao na makaburi yao. Wakoloni wa Kizungu hawakukuta Waislamu Waafrika wenye kisomo cha juu, yaani madaktari na wenye shahada za chuo kikuu. Waliokuwa wamesoma walikuwa na kisomo cha awali.
Wakati huo wote Waarabu na Waislamu walikuwa wanafanya nini, Waislamu wasisome na kuendelea? Je, walikuwa wanawangoja kwanza Wakristo wafike, ndipo mbiyo za maendeleo zianze? Mwalimu Nyerere Baba wa Taifa alikuta mambo yameshaharibika. Alichofanya ni kurekebisha makosa yaliyofanywa na utawala wa Warabu.
Chakushangaza, kikundi hiki kinachoshambulia wakoloni wa Kizungu, Wakristo na Mwalimu Nyerere, hakielezi hata kidogo kuhusu ukoloni wa Kiarabu ambao ndio waliokuwa watawala wa mwanzo wa Tanganyika kabla ya Wazungu. Na ndiyo waliotawala kwa kipindi kirefu kupita wote. Hakielezi mema na mabaya waliyofanya Warabu. Kwao, historia ya Tanganyika inaanzia wakoloni wa Kizungu, na utawala wa Mwalimu Nyerere. Utafikiri kuwa Mwarabu hajawahi kuishi hapa Tanganyika.
Ndugu hawa pia hawaelezi, chimbuko la lugha ya Kiswahili; ni, Kwanini kina maneno mengi ya Kiarabu? Kwa nini maandishi yote ya kale, tungo za mashairi na za mambo mbalimbali yaliandikwa kwa lugha ya Kiswahili lakini kwa herufi za Kiarbu? Kwa nini Tanganyika haina urithi wa baadhi ya Wataalamu; wala, hatusomi habari za wataalamu na watu mashuhuri wa kiafrika waliokuwepo wakati wa ukoloni wa Waarabu.
Historia ya Tanganyika haisemi juu ya wataalamu waliosoma wakati wa enzi ya Waarabu, hapa Tanganyika, na waliopelekwa katika nchi za Kiarabu kusoma. Kama tulivyoona wakati wa Utawala wa kizungu, watu walisoma hapa na waliofanya vizuri walienda Ulaya kwa masomo ya juu. Kwa nini, Tanganyika hakuna mambo ya kimaendeleo yaliyoachwa na utawala wa Kiarabu?
Waliodidimiza elimu na maendeleo ya Waislamu ni Warabu walioleta dini ya, Kislamu na dini ya kwanza ya kigeni Tanganyika na watawala wa kwanza wa Tanganyika. Uislamu na Waarabu wanatoka nchi za Mashariki ya Kati, nchi za kwanza kimaendeleo ulimwinguni. Waarabu waliendelea kabla ya Wazungu. Lakini kwa miaka zaidi ya 1000 wakiwa hapa Tanganyika, hakuna walichofanya cha maana, zaidi ya kuendesha biashara ya Utumwa na kuleta dini ya Kiislamu. Tanganyika tunawakumbuka Waarabu kwa mambo hayo mawili tu. Warabu hawakuelemisha wala wahakuwa na mpango wa kuwatibu Waafrika.
Kuanzia karne ya saba, Uislamu ulipofika hapa Tanganyika mapaka karne ya 19, wakoloni wakizungu na Ukristo ulipofika. Kama Waarabu, wangalikuwa watu wa maendeleo, Wazungu na Wakristo wangaliikuta nchi hii imeendelea kama nchi za Afrika ya Kaskazini na nchi za Mashariki ya Kati. Wangaliikuta nchi hii ina vyuo vikuu na idadi kubwa ya maprofesa. Sasa hivi tungekuwa na maendeleo sawa na Iran, Libya na nchi nyinginezo zinazotawaliwa na serikali za Kiislamu.
Kuna kitabu kilichoandikwa na Mwalimu Hussein Bashir; kinachoitwa, “Historia ya Uislamu Pwani ya Azania. Kukua na kuondoka kwa dola ya Kilwa.” Mtaalamu huyu ameandika mambo ambayo si kubaliani nayo na ninaamini na hata, wewe utakayesoma kitabu chake hutakubaliana naye, kwa kuwa hakuna ushahidi wa mambo aliyoandika, na nivigumu kuyasadiki. Mwalimu Bashir ameandika mengi lakini nimechagua machache kutoka ‘Sehemu ya Tano,’ ya kitabu chake. Nitanukuu machache kutoka uk.53 na 54, anaandika:
“Pia vijana waliofaulu (katika shule za awali za Kiislamu zilizokuwa zimetapakaa katika miji yote ya Tanganyika). walifanikiwa kwenda kusoma katika vyuo vikuu vilivyoko Andalus (Hispania), Baghdad, Iraq, Al Azhar (Misri), Chuo Kikuu cha Timbuktu Afrika ya Magharibi, Alzaitun (Tunisia), na Alkarakuyiri (Fez-Morocco). Mfano wa vijana waliofanikiwa kwenda kusoma katika vyuo hivyo ni pamoja na Hassan Hamisi Mwinyi Sembe Shomvi kutoka katika kijiji cha mpinga, Bagamoyo, alitokea katika shule ya awali ya Mbweni na kwenda kusoma chuo kikuu cha madawa na tiba cha Ibn Sina (Aveccina) cha Iraq.
Na pindi aliporudi nchini alikwenda katika kijiji cha kihistoria cha Makurunge (Bagamoyo), ambapo alianzisha shule ya Tiba na madawa.”
“Shule hiyo ya Sayansi na Tiba ya Makurunge ilipofikia karne ya kumi na saba katikati iliweza kutoa mabingwa walioshiriki operesheni ya kwanza ya upasuaji wa tumbo lenye saratani, iliyofanyika Iraq katika mji wa Nasriyah. Operesheni hii ilishirikisha madaktari bingwa 136 wakiwemo Waislamu kutoka Pwani yetu, kutoka katika miji ya Bagamoyo, Kaole, na Tumbatu. Ni katika mafanikio haya ya elimu ya Afya na uchumi, ndipo Dola Kilwa ilipata kuvuma duniani kwa vila shule zote za elimu ya awali zipatazo 16,689, shule za msingi 13,106 vyuo vya elimu ya juu 38 viliweza kutoa wanataaluma walioweza kutetemesha dunia kitaaluma.”
Kama hizo takwimu ni za kweli, ni kweli, kwa wakati huo dunia ingetetemeka. Na maendeleo makubwa kama haya nchi hizo zilizotetemeshwa zisingeweza kuacha kuandika. Mbona taarifa ya biashara ya Kilwa zinapatikana katika nchi nyingine zilizokuwa zinafanya biashara na Kilwa. Lakini hazitaji mafanikio haya ya kutisha ya elimu. Huyo mtaalamu Ibn Swaleh anaandika maajabu ya Pwani ya Tanganyika bila mwenyewe kufika. Je! Alizipata wapi? Na wewe mwalimu Bashir unaye sambaza maandishi haya unauhakika kuwa ni za kweli? Hebu wahakikishie Watanzania uhalali wa utafiti wako.
Habari kama hizi ndizo zinazo watia kichaa vijana wa Kiislamu. Wanaamini kuwa Wakoloni wa Kizungu ambao pia ni Wakristo ndiyo waliohujumu maendeleo ya Waaislamu. Uongo kama huu uko wazi kabisa kuwa ni uongo nayeye anayesambaza anajuwa kuwa anaeneza uongo. Wala siyo kueneza uongo tu bali zinachochea chuki.
Tatizo linakuja hapa, hayo maendeleo makubwa ambayo mwandishi wetu anayasifia, maendeleo yaliyodumu kwa kipindi cha miaka kama 1200 tangu Uislamu ulipoingia; yalienda wapi mpaka Mjerumani asikute kitu. Wasikute hata shule moja ya msingi ukiondoa shule za kati na vyuo vikuu na hospitali zilizokuwa zimetapakaa katika miji yote ya pwani. Je huyu mtawala alipotoroka alibeba au alibomoa majengo yote ya shula na hospitali. Je, walimu nao alienda nao. Kama wlimu nao walitoroka je maelfu ya watu waliosoma katika shule hizo na vyuo hivyo nao walitoroka, mpaka Wajerumani wakakuta watu wana elimu ya awali tu. Ndipo Wajerumani wakaanza kuwasomesha Waislamu elimu ya uhakika mpaka Wakristo nao wakataka wasomeshwe nao na serikali kama wenzao Waislamu. Shule za awali za Kiislamu husomeshewa misikitini. Zaidi sana husomesha dini ya Kiislamu; kusoma Kurani na kuandika Pia hufundisha maadili ya Kiislamu. Shule hizi zipo mpaka leo. Hata kanisa lilikuwa na shule za awali walizofundishia waumini wao kusoma na kuandika.
Ushahidi wa kuwa Waarabu walifanya biashara ya utumwa upo mpaka leo. Visalia vya Watumwa vipo mpaka sasa. Vizazi vya watumwa waliokombolewa kutoka majahazi ya Waarabu wakisafirishwa kwenda kuuzwa nchi za nje bado wapo hawajatoweka. Mahandaki waliyokuwa wanahifadhia watumwa, nyakati za usiku wasije wakatoroka yapo. Vituo vya Wafanyabiashara ya Utumwa vingine bado vipo katika barabara la kusafilishia watumwa kutoka bara kwenda pwani. Hata masalia ya Waarabu wapo mpaka leo hii katika vituo hivi. Kioja ni kutoweka kwa shule, vyuo vikuu, walimu, watu wote waliosoma katika vyuo vikuu 38 na shule za msingi 13106. Vyuo na wataalamu wake walienda wapi? Hospitali, madakitari na watumishi wengine walienda wapi? Je, wataalamu waliohitimu katika vyuo vikuu 38 walifanya nini cha maendeleo? Au walisoma bila kufanya chochote cha maendeleo? Cha kushangaza ni kuwa anaeleza kwamba zilikuwepo lakini haelezi zilienda wapi? Zilikumbwa na mikasa gani? Na ni lini mambo hayo yalitokea?
Mohammad Ibn Abdullah Ibn Batuta alipotembelea Dola hili aliandika taarifa nyingi juu ya Dola hii ikiwemo inayo husu wizara hii ya elimu na sekta ya elimu kwa ujumla wake. Aliandika:
“Mwanachuoni huyo, Ibn Batuta, Uk.53, ameeleza kuwa, uongozi wa miji ya Kiislamu ya Kaole Bagamoyo za wakati huo, uliandaa makao makuu ya kutengeneza na kutasfisiri ‘mitaala ya shule za awali’, kwa kupitia chuo cha walimu wa awali kilichopo pwani ya Sheikh Mussa Hassan (Msasani).”
Alichoona Batuta ni jopo la kutafsiri mitaala ya shule za awali kwa kupitia chuo cha walimu wa shule za awali. Hizi ndizo shule zilizokuwepo na bado zipo. Zipo chini ya misikiti. Ingawaje sasa haziitwi shule za awali, bali Madrassa. Huu ndio ukweli. Katika mambo aliyosifia Batuta ni biashara ya kimataifa. Iliyostawi na, uzuri wa miskiti, ukarimu watu, pia alipendezwa na lugha ya Kiswahil.
Mwandishi wa kitabu hiki anataja majina ya wanafunzi waliokwenda kusoma Mashariki ya kati kutoka shule za awali na kuiingia chuo kikuu cha Iraki. Nanukuu:
Pia vijana waliofaulu walifanikiwa kwenda kusoma katika vyuo vikuu vilivyopo Andalus (Hispania), Baghdad, Iraq, Al Azhar (Misri) Chuo Kikuu cha Timbuktu Afrika ya Magharibi, Alzaitun (Tunisia), na Alkarakuyiri (Fez-Morocco). Mfano wa vijana waliobahatika kwenda kusoma katika vyuo hivyo ni pamoja na Hassan Hamisi Mwinyi Sembe Shomvi kutoka katika kijiji cha Mpinga, Bagamoyo, alitokea katika shule ya awali ya Mbweni, na kwenda kusoma chuo kikuu cha madawa na tiba cha Ibn Sina (Aveccina) cha Iraq.
Haiwezekani mtu aliyesoma shule ya awali kwenda moja kwa moja na kuingia chuo kikuu. Ningeamini kama angalisema kuwa huko Iraq walisoma kwanza shule nyingine, kabla ya kujiunga na vyuo vikuu.
Pia si kweli kuwa maendeleo ya Mashariki ya kati ni matokeo ya Uislamu. Nabii Muhamad alizaliwa mwaka wa 575 na alianza kuhubiri Uislamu mwaka 610 AD. Hata hvyo tarehe rasmi ya mwanzo wa Uislamu ni 622. Wakati Mashariki ya Kati waliendelea zamani sana Kabla ya Ibrahim. Wakati Yusufu alipofika Misri alikuta Wamisri wameendelea. Waisraeli walipokuwepo Misri wakitumika kama Watumwa ndio waliojenga Mapiramid, yanayoonekana mpaka leo. Tangu wakati huo Wamisri walikuwa wanajuwa kuhifadhi maiti kwa muda mrefu.
Waislamu na Waarabu ni vitu viwili tofauti. Uislamu ni dini na Waarabu ni taifa. Maendeleo ya Waislamu yalitokea katika taifa la Waarabu waliokuwa wameendelea tayari. Ni kweli kuwa wakati Warabu wakiendelea Wazungu wa Ulaya walikuwa bado nyuma sana. ni nini kilichotokea mpaka Wazungu wakaendelea na Waarabu wakabaki nyuma? Wewe mtaalamu wa kugundua mambo ya kale, hebu tafiti ni wapi Waarabu walipojikwaa mpaka wakapitwa na Wazungu?
Kuna uongo mwingine unaozagaa pia; unasema kuwa Ulaya yote ilikuwa chini ya utawala wa Kiislamu. Ulaya yote hii si kweli hata kidogo. Jamaa anasema kuwa walioandika Historia ni Wazungu, kwa hiyo walipotosha Historia, ndiyo maana wanataka kuandika upya Historia, yaani kufuta ukweli na kutia uongo, kama walivyoanza sasa.
Katika karne ya 7 na 8 Uislamu ulienea kwa haraka sana. Ulienea kwa kasi kwa njia mbili, njia ya kwanza ni kwa watu kuupokea Uislamu kwa hiari yao, kama ilivyokuwa hapa Afrika ya Mashariki. Njia ya pili ni kwa vita. Nchi zote zilizotekwa na Waislamu watu wake wliingia Uislamu; lakini nchi zile ambazo hazikutekwa na Waislamu watu walibaki na dini zao. Uislamu ulianzia huko Macca Saud Arabia.
Kwa kipindi cha miaka 25 Nabii Muhamad na wafuasi wake waliweza kuteka na kutawala karibu nchi zote za Kiarabu. Kwa haraka Uislamu ulichukuwa nafasi ya tatu katika dini kuu za dunia zenye chimbuko la Ibrahimu; ambazo ni Judaism (dini ya Kiyahudi) na Ukristo. Mpaka mwaka wa 650 Waislamu walitawala Arabia, Iraq, Syria, Lebanon, Palestine na Misri.
Katika mwaka 733 miaka 100 baada ya kifo cha Nabii Muhammad, Uislamu ulienea na kutawala toka China India Afrika ya Kaskazini; mpaka ukafika Spain Ulaya Magharibi. Majeshi ya Waislamu yaliendelea mbele mpaka yakafika Magharibi ya Ufaransa. Majeshi ya Uislamu yalipoingia Ufaransa Magharibi, ndipo yalipozuiwa na jeshi la Mfalme Charles wa Ufaransa. Charles ndiye aliyewazuia Waislamu wasiingie na kuteka nchi za Ulaya. Nchi za Ulaya hazijawahi kutawaliwa na Waislamu kama porojo hizo zinavyoendelea.
Watu kama hawa wanaotunga uongo halafu wenyewe walioutunga wanauamini na kuutetea na kuanza kuueneza kwa watu wasio juwa na wala hawana uwezo wa kupata ukweli. Hawa ndio wachochezi wabaya. Wanawafanya vijana kujiingiza katika vitendo viovu wakiamini kuwa wanahaki. Wanatetea haki zao na dini yao. Kumbe wanatetea uongo. Serikali inaweza ikawatuliza wasiendelee kufanya fujo; lakini hawatafuta imani yao ya kuwa wanaonewa, mpaka watakapoelezwa ukweli. Ni jambo baya sana kutumia uongo kutetea dini ili iweze kukubalika. Dini inatetewa na ukweli, unyofu wa maisha ya wafuasi wake, na vitendo inavyoendana na maandiko yao yaani kutii maandiko ya dini.
KUFIKA KWA WARENO TANGANYIKA
Mreno, mgunduzi, Vasco da Gama, alifika kwa mara ya kwanza katika pwani ya Tanganyika mwaka 1498. Alikuwa akitafuta njia ya kufika India. Aliipata na alifika India. Da Gama alipofika pwani ya Tanganyika alikuta Waarabu waliokuwa wanaishi katika miji ya pwani ya Tanganyika na Waafrika walikuwa wameshasilimu. Waafrika, Watanganyika wa pwani, waliosilimu, waliofuata ustarabu na utamaduni wa Kiislamu, unaofanana na wa Kiarabu. Kwa sababu walishi na Warabu kwa kipindi cha karne nyingi. Miji aliyoitembelea ilikuwa na utawala mathubuti, biashara za kimataifa zilizostawi na kuendelea. Kulikuwa na bandari nzuri. Mabaharia wa Afrika Mashariki walifika mpaka China.
Watu mashuhuri kutoka miji ya pwani ya Tanganyika, waliwatembelea wageni wao Wareno. Wenyeji hawa hawakushangaa kuona Wazungu na meli; bali waliwatazama kwa kiburi na kwa dharau. Walipopewa zawadi, walidharau. Inaonekana kuwa walishawahi kupewa zawadi kubwa kuliko hizo walizopewa. Pia walishaona meli kubwa zaidi kupita meli alizokuja nazo Dagama. Hii inaonyesha kuwa walikuwa wamezoea kutembelewa na wageni kutoka sehemu mbalimbali za ulimwengu. Katika ukanda huu biashara kubwa zaidi ilikuwa kati ya India, Uajemi, Arabia na Afrika Mashariki. Kiini cha biashara hii ilikuwa Uajemi.
Mwaka wa 1502 Dagama alifika Kilwa. Huko alikutana na wanawake 200 waliotaka aende nao Ureno wakawe Wakristo. Wanawake hao walikuwa wake wa Waislamu. Dagama alikataa. Alihofia kushindwa kuwadhibiti mabaharia wake mbele ya kundi hilo la wanawake. Alipowakataa baadhi ya wanawake walijitupa katika maji ili waogelee, wapande meli, waende Ureno wakawe Wakristo. Sultan wa Kilwa alimwambia Dagama kuwa wanawake 40 walikuwa tayari wameachwa na waume zao kwa kutaka kuingia Ukristo; kwa hiyo kama hataenda nao maisha yao yatakuwa hatarini. Kwa hiyo Dagama akaenda nao Ureno. Huko wakabatizwa. Hawakurudi, walibaki huko, wakawa Waafrika wa kwanza kubatizwa. Wanawake walio kwenda Ureno, walishi huko, walikuwa raia wa Kireno. Walikuwa huru kama Wareno wenyewe. Wareno hawakuwa na ubaguzi wa aina yoyote ile. Wanawake hawa waliishi huko maisha yao yote. Wasingaliweza kurudi Tanganyika kuhofia maisha yao. Kwa kuwa ndugu zao wote walikuwa Waislamu.
Mwaka 1505, Kilwa ilitekwa na Wareno. Shirika la Kikristo, la Kiroma, la Wafrancisko. Walienda kufanya kazi ya Umisionari huko Kilwa. Baada ya Wakilwa kusikia Injili, watu wapatao 40 walitaka kubatizwa; lakini Wareno walikataa kwa kuwa walikuwa watumwa mali ya watu.
Mwaka 1512,Wareno waliondoka Kiwa na hawakurudi tena Kilwa. Na Wakristo waliobatizwa huko Kilwa wakapotea, kwa kuwa hawakuwa na watunzaji. Katika kipindi cha miaka 80 ya kwanza ya utawala wa Kireno katika Afrika Mashariki. Wamishonari walifanya kazi ndogo sana. Hakukuwa na watu wengi waliobatizwa.
Huko Zanzibar, wamishonari walipata Wakristo kwa kununua watoto na vijana watumwa waliotaka kuingia Ukristo na ambao, mabwana zao walitaka kuwauza. Wamishonari waliwanunua kabla ya kuuzwa kwa watu wengine; ambao wangeendeleza utumwa wao. Walipowanunua waliwabatiza na waliwaacha huru na kuwatunza katika nyumba za watawa. Baadhi yao walipelekwa Ureno. Mpaka mwaka 1624, Zanzibar ilikuwa na Wakristo wachache sana. Kwa kuwa kila mara waliotaka kuingia Ukristo ni watumwa, si Waafrika huru wala Warabu.
Kazi ya Wareno ya kueneza Injili Afrika Mashariki ilikuwa ngumu na ya hatari sana. Kwa kuwa Warabu hawakuruhusu Ukristo uingie Afrika ya Mashariki. Ingawaje Wareno walijitoa muhanga, kueneza Injili na kubatiza wachache; lakini hata hao wachche waliobatizawa hawakudumu. Waliobaki waliingia katika taifa la Kireno na kuwa Wareno, na wengine walirudi kwenye Uislam.
error: Jisajili kupata uhuru zaidi !!