KAZI YA NYUMBANI DARASA LA SITA APRILI 2021 + MAJIBU

By , in DRS 1-7 on . Tagged width:

SEHEMU A: METHALI NA MAANA ZAKE

Kwa kila kifungu cha maneno kati ya hivi vifuatavyo unda methali moja tu ya Kiswahili ambayo inawiana na maelezo yanayohusika.

  1. Ni muhimu katika maisha kushirikiana na wenzetu kwa kila jambo ili kupata mafanikio.

            METHALI _________________________________

2. Afadhali kupata moja na kujiondokea kuliko kusubiri kumi ambazo kila ukienda huzipati.

            METHALI _________________________________

3. Aghalabu kila kipya hupendwa hata kama upya huo ni mbaya.

METHALI _________________________________

4. Usisahau hali yako duni ya zamani kwa sababu ya hali yako bora sana uliyonayo sasa.

METHALI _________________________________

5. Kwa kawaida mtu anayejishughulisha na uvuvi wa pwani hawezi kukosa kitoweo, hata akikosa kingi kidogo atapata

METHALI _________________________________

6. Mtu mwenye kuonesha uhodari mwingi katika jambo aghalabu kutokea kuharibu.

METHALI _________________________________

7. Anayefurahishwa na kitu chochote au mtu yeyote, huweza kuona tu uzuri wa hicho kitu au huyo mtu.

METHALI _________________________________

SEHEMU B: MATUMIZI YA NENO MOJA

Andika neno moja linalojumuisha maneno yafuatayo

8. Mchicha, kabichi, spinachi, majani ya kunde, kisamvu na matembele______________

9. Tanzania, Uingereza, Ghana, China, Kenya, Malawi na Marekani_________________

10. Kijiko, kikombe, kisu, sufuria ______________________

11. Chuma, shaba, dhahabu, almasi, rubi, bati, risasi na Tanzanaiti______________

12. Meza, kiti, kabati, kitanda ______________________

 

MAJIBU

1. Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu
2. Heri kenda shika kuliko kumi nenda rudi
3. Kipya kinyemi japo ni kidonda
4. Usiache mbachao kwa mswala upitao
5. Mgaagaa na upwa hali wali mkavu
6. Ujanja mwingi mbele giza
7. Moyo ukipenda chongo huita kengeza
8. Mboga
9. Nchi/Taifa
10. Vyombo
11. Madini
12. Samani

error: Jisajili kupata uhuru zaidi !!