KANUNI YA AKIMEDES YA UELEAJI 

By , in Sayansi kwa Kiswahili on .

Vilevile aligundua kanuni ya ueleaji inayoitwa pia “kanuni ya Akimedes” kuwa “gimba linalowekwa katika kioevu husukumwa juu kwa nguvu iliyo sawa na uzito wa kioevu kinachosogezwa kando na gimba hili”. Alingundua kanuni hii alipopewa kazi ya kufanya utafiti kama taji la mfalme wa Siracusa lilikuwa dhahabu tupu au kama dhahabu ilizimuliwa kwa kuchanganya na fedha. Hapa kuna hadithi ya kwamba aliona usuluhisho siku moja alipooga bafuni akiona jinsi maji yalivyopanda juu alipoingia ndani yake. Hapa Akimedes alielewa ya kwamba aliweza kupata mjao wa taji kwa kuizamisha katika maji. Kwa kupima mjao na uzito aliweza kugundua kama taji lilikuwa dhahabu tupu au la kwa sababu aliweza kulinganisha kiasi cha mjao wa dhahabu tupu chenye uzito uleule.

SHERIA YA UELEAJI

Kitu kikizamishwa nusu au chote kwenye ugiligili, hukutana na kani mnyanyuo ambayo ni sawa na uzito wa ugiligili uliochukuliwa nafasi.

LAW OF FLOATION

When a body is partially or fully immersed in a fluid, it experiences an upthrust which is equal to weight of fluid displaced.

KANUNI YA AKIMEDES

Kitu kikizamishwa nusu au chote kwenye ugiligili, ujazo wa kitu kilichozama huwa sawa na ujazo wa ugiligili uliochukuliwa nafasi.

ARCHIMEDES PRINCIPLE

When a body is partially or totally immersed in a fluid, the volume of a body immersed equals to the volume of fluid displaced.

Facebook Comments
Recommended articles