KAMUSI YA NDEGE WA TANZANIA

By , in Kamusi on . Tagged width:

NDEGE (BIRDS, AVES)

Askari (soli)
Martial Eagle
Polemaetus bellicosus
Ndege mkubwa mla nyama wa jamii ya tai; mgongoni ni kahawia-kijivu, kifua na kichwa cheusi na tumbo jeupe lenye madoadoa. Ana kisunzu kipana kisichotokeza sana.


Kielelezo Na. 1 Askari

Babewana
Verreaux’s Eagle Owl
Bubo lacteus
Bundi mkubwa kahawia-kijivu mwenye miraba midogo, utosi na masikio meusi, mraba mweusi kando ya uso na macho ya maziwa.

Barabara
Fiscal Shrike
Lanius collaris
Kipwe mwenye mkia mrefu kiasi, mweusi, mwenye pembe na shina jeupe, koo na tumbo nyeupe, yiu mweusi na ana kiraka cheupe begani (Tazama Kipwe).

Baruwai
Little Swift
Apus affinis
Aina ya Mbayuwayu mdogo mwenye takojeupe na mkia mfupi usio na ncha mbili kama ya wenzake.

Bata
Duck
Anatidae
Ndege wa aina, ukubwa na rangi mbalimbali wa jamii na waliofanana na bata afugwae, waishio kwenye maziwa.


Kielelezo Na. 2 Babewana

Bata Bukini
Goose
Anatidae
Kama bata lakini hawa wanapendelea kula kandokando ya maziwa na wakati wa mvua wanaweza kuonekana mbugani, mbali na maziwa.

Bata Bukini-nyundo
Knob-billed Goose
Sarkidiornis melanotos
Huyu ana nyundo juu ya domo lake.

Bata Miti
Tree Duck
Dendrocygna
Kama bata lakini hawa wana shingo ndefu zilizonyooka juu na mara kwa mara hupendelea kukaa juu ya miti, kando ya maziwa na mito.


Kielelezo Na. 3 Baruwai

Bata Miti-kahawia
Fulvous Tree Duck
Dendrocygna bicolor
Bata-miti wa kikahawia-cheusi juu na tumbo kahawia, mwenye mraba mweusi nyuma ya shingo, milia meupe mipana ubavuni na kisunzu kidogo.

Bata Miti-mweupe
White-faced Tree Duck
Dendrocygna viduata
Ni bata pekee mwenye uso mweupe. Rangi yake ni ya kikahawia-cheusi. Ana kichwa cheusi, tumbo jeusi na milia meusi mbawani.


Kielelezo Na. 4 Bata

Bendera-kahawia
Cinnamon-breasted Bunting
Fringillaria tahapis
Ndege wadogo kahawia wajamii ya chiruku, walao nafaka, wenye tumbo kahawia na miraba myeupe na myeusi kichwani.

Bendera-njano
Golden-breasted Bunting
Emberiza flaviventris
Huyu ana tumbo la njano.

Biliwili
African fire finch
Lagonosticta rubricata
Aina ya Mtolondo mkubwa kiasi, mwekundu, mwenye mbawa za kikahawia, domo la kijivu na manyoya ya chini ya mkia meusi.

Bintichuma-koojeusi
Spectacled Weaver
Hyphantargus ocularis
Kama yule njano lakini dume lina koo jeusi, na ni mdogo. (Tazama Mnaana).

Bintichuma-mwekundu
Golden Palm Weaver
Ploceus bojeri
Huyu ana kichwa chekundu

Bintichuma-njano
Golden Weaver-Holub’s
Xanthophilus xanthops
Ni mnaana mnene wa njano, aliyefanana na Umbia lakini huyu ana domo la kijivu na macho ya njano wakati ya Umbia ni ya rangi ya chungwa.


Kielelezo Na. 5 Bata Bukini


Kielelezo Na. 6 Bata Bukini-nvundo

Bluu-upande
Hottentot Teal
Anas punctata
Bata mdogo kuliko wofe mwenye kofia nyeusi na rangi ya bluu pembeni mwa domo lake.

Bundi
Owl
Strigidae
Ndege wakubwa kiasi, pekee wenye nyuso mviringo zenye macho kama ya binadamu na masikio yaliyotokeza kama ya mnyama. Wana kilio cha kutisha ambacho watu wengi huamini kinaambatana na balaa. (Tazama Babewana)


Kielelezo Na. 7 Bata Miti-kahawia

Bundi-kahawia
African Marsh Owl
Asio capensis
Bundi mkubwa kiasi wa kikahawia mwenye macho ya kikahawia-cheusi, pua nyeusi na masikio madogo sana. Anapendelea mabwawa ya nyika. Yuko mwenzake wa msituni (Wood-owl) mwenye pua ya njano.


Kielelezo Na. 8 Bata Miti-mweupe

Bundi-mwekundu
White-faced Scops Owl
Otus leucotis
Huyu ni wa kijivu-cheusi chenye milia na madoa maridadi. Ana uso mweupe na macho mekundu.

Bundi-mweupe
African Scops Owl
Otus scopus
jamii ya Bundi-mwekundu mwenye macho meupe.


Kielelezo Na. 9 Bendera-kahawia

Bwabwaja
Pratincole
Glareola pratincola
Ndege mdogo kahawia wa kando ya maziwa, aliyefanana na Membe, mwenye koo la njano na mkia wenye ncha mbili ndefu kama wa Mbayuwayu.


Kielelezo Na. 10 Biliwili

Bwenzi
Wattled Crane
Bugeranus carunculatus
Taji mwenye shingo nyeupe na dehedehe ndefu zenye manyoya. (Tazama Taji).


Kielelezo Na. 11 Bluu-upande

Chambogo-kijivu
Vieillot’s Black Weaver
Melanopterix mgerrimus
Mnaana mweusi mwenye domo la kijivu najicho la njano.

Chambogo-njano
Buffalo Weaver
Bulbalornis albirostris
Kama yule kijivu lakini ni mkubwa na domo lake ni la machungwa.


Kielelezo Na. 12 Bwabwaja

Chamchanga
Sandpiper
Scolopacidae
Ndege wakubwa kiasi waishio kando ya maji, na wa rangi mbalimbali, waliofanana na Kiluwiluwi lakini hawa miguu na midomo yao ni mirefu na myembamba. Wana vidole vinne badala ya vitatu kama vya Kiluwiluwi.


Kielelezo Na. 13 Chambogo-kijivu


Kielelezo Na. 14 Chamchanga

Chati
Stone-chat
Saxicola torquata
Jamii ya Kurumbiza ambaye ana kichwa, mbawa na mkia mweusi. Ana kiraka cheupe begani, mbawani na matakoni na doa kubwa jekundu kifuani. Ni ndege wa mbuga za milimani.

Chekeamwezi
Curlew
Numenius arquata
Ndege wa kijivu-njano wa kando ya maziwa na bahari mwenye miguu mirefu, domo refu sana lililopindia chini na tako jeupe.

Chekeamwezi-mdogo
Sandpiper Curlew
Calidris testacea
Kama Chekeamwezi lakini huyu ni mdogo na tumbo lake jeupe.


Kielelezo Na. 15 Chati

Chekechea
Widow-bird
Coliuspasser
Ndege wakubwa kidogo weusi wa jamii ya chiriku baadhi yao wenye mikia mirefu Sana na mbawa zenye unjano-mweupe kidogo. (Tazama Mleli).

Chekechea-mwekundu
Fan-tailed Widow bird
Coliuspasser axillaris
Huyu ana baka la kikahawia-chekundu begani na mkia wa kawaida.

Chekechea-mweupe
White-winged Widow bird
Coliuspasser albonotatus
Kama Chekechea-mwekundu lakini ana baka la kikahawia na jeupe begani.

Chekehua
Spurwing Plover
Hoplopterus spinosus
Kiluwiluwi mkubwa mwenye kisunzu kidogo cheusi, mgongo kahawia, shingo nyeupe na tako jeupe. Ubawa wakc una ukucha nchani.


Kielelezo Na. 16 Chekeamwezi

Chekehukwa
Ruff
Philomachus pugnax
Jamii ya Kiguunina mwenye miguu ya njano natako kahawia, jeupe pembeni.

Chepeo (Kanga)
Helmeted Guinea Fowl
Numida mitrata
Ni yule Kanga wa mbugani mwenye ushungi mithili ya upembe kichwani.

Cherimiyo
Black and White Fly-catcher
Platysteira cyanea
Ni Shore mweusi juu na chini mweupe mwenye ngozi nyekundu inayozunguka jicho na mraba mweupe wa mbawa. Jike lina kifua chekundu na dume lina mraba mweusi kifuani.


Kielelezo Na. 17 Chekehua

Cherero
Budgerigar
Melopsittacidae
Kasuku mapenzi mdogo anayefugwa, wa kijani na njano mwenye mkia mrefu.

Cheruku
Temminck’s Courser
Cursorius temminckii
Ndege jamii ya Bwabwaja, aliyefanana zaidi na Kiluwiluwi lakini mdomo wake mdogo umepindia chini kama wa Sululu. Ana mgongo mweupe, kofia ya kijivu kichwani, tumbo lenye kiraka cheusi, na mraba mweusi jichoni.


Kielelezo Na. 18 Chekehukwa

Cheusi (Nderi)
Verreaux’s Eagle
Aquila verreauxii
Tai mkubwa mweusi. Akiinua mbawa, tako lake na mgongo huonekana mweupe.

Chigi
Yellow-fronted canary
Serinus mozambicus
Ni Chiriku kahawia mgongoni, mwenye utosi na tako la njano iliyokolea. (Tazama Msilimiwa).

Chiriku (Msili)
Canary
Fringillidae
Ndege wadogo wa kijani-kijivu wa jamii ya Mtolondo (Finch) wenye tumbo njano, miraba ya njano juu ya jicho na milia ya njano mbavuni. (Tazama Msilimiwa).


Kielelezo Na. 19 Chepeo

Chiru
Ground-scraper Thrush
Turdus Litsipsirupa
Aina ya Mkesha wa kahawia-kijivu mwenye tumbo jeupe, madoa mengi na mkia mfupi kiasi.

Chokiro
While-eyed Slaty Flycatcher
Dioptrornis fischeri
Shore kijivu mwenye mkia wa kawaida na mviringo mpana mweupe kuzunguka jicho.


Kielelezo Na. 20 Cherimiyo

Chole
Greenbul
Picnonotidae
Ndege mdogo kijani-chekundu wajamii ya Shore na Teleka.


Kielelezo Na. 21 Cheruku


Kielelezo Na. 22 Cheusi

Chole-mwekundu
Red-tailed Greenbul
Tricophorus calurus
Huyu ana mkia mwekundu

Choleulingo
Yellow-whiskered Greenbul
Stelgidocichla latirostris
Chole wa kijani-chekundu mwenye mraba wa njano shavuni.

Chopoa (Mvuvi)
King-fisher
Alcedinidae
Ndege wakubwa kiasi wa jamii ya Mtilili wenye midomo mipana na mirefu iliyochongoka mbele ambao huvua samaki.


Kielelezo Na. 23 Chiru

Chozi (Mlaasali)
Sunbird
Nectarinidae
Ndege wadogo wenye rangi mbalimbali za kupendeza na midomo mirefu myembamba iliyopindia chini wanaokula asali katika maua. (Tazama Neli)

Damisi
Black-lored Babbler
Turdoides hypoleuka
Jamii ya Mpayupayu, wa kijivu, mwenye doajeusi mbele ya jicho na milia meusi na meupe kooni.

Denge
White-bellied Go-away
Corythaixoides leucogaster
Ndege mkubwa kijivu wa jamii ya Dura mwenye tumbo jeupe na manyoya marefu kama kisunzu utosini. Hulia ‘go-away.’


Kielelezo Na. 24 Chole-mwekundu

Detepwani
Pied King-fisher
Ceryle rudis
Chopoa mdogo wa kijivu mwenye kusunzu kidogo cheupe, miraba miwili meusi penye tumbo lake jeupe, mraba mweupe juu ya jicho na milia mingi myeusi mgongoni.

Domojuu (Shembea)
Avoicet
Recurvirostra avocetta
Ndege mweupe wa kando ya maziwa ya chumvi mwenye kichwa cheusi, miguu mirefu ya kijivu-cheusi, miraba mitatu myeusi ya mkato mgongoni na domo refu jeusi lililopindia juu.


Kielelezo Na. 25 Chopoa

Domokijiko
African Spoonbill
Platalea alba
Korongo mweupe mwenye miguu na uso mwekundu na domo refu lililopanuka kama kijiko nchani.

Domongazi
Saddle-bill Stork
Ephippiorynchus senegalensis
Korongo kahawia-kijivu mwenye kichwa na shingo nyeusi, bega na tumbo jeupe, vidole na magoti mekendu na domo refu lenye rangi tatu; yaani njano juu, nyeusi katikati na nyekundu nchani.

Domowazi
Open-bill Stork
Anastomus lamelligerus
Korongo kahawia-kijivu mwili mzima mwenye domo refu la kijivu lenye mwanya katikati.


Kielelezo Na. 26 Denge

Dudumizi
White-browed Coucal
Centropus superciliosus
Ndege mkubwa mwenye mkia mrefu wa kijivu, mbawa kahawia, miraba myeusi ya kukata mgongoni na myeupe ya kuteremka shingoni, domo na kichwa cheusi na msitari mweupe juu ya jicho. Mlio wake wa ‘Du-du-du-du-du’ vichakani husemekana ni ishara ya kuja kwa mvua.

Dura
Turaco
Musophagidae
Ndege mkubwa wa msituni wa rangi mbalimbali wenye visunzu na mikia mrefu. Walio wengi ni kijani mgongoni na tumboni, na wana miraba myekundu kando ya mbawa. (Tazama Shorobo).


Kielelezo Na. 27 Detepwani

Fimbi-kahawia
Crowned Hornbill
Tockus alboterminatus
Hondohondo mkubwa kiasi wa kahawia, wa nyika na milimani. Ana domo jekundu lenye mundu mdogo, kisunzu kidogo kisogoni na ncha nyeupe mkiani.


Kielelezo Na. 28 Domojuu


Kielelezo. Na. 29 Domokijiko

Fimbi-mwekundu
Red-billed Hornbill
Tockus erythrorhynchus
Huyu ana domo jekundu na madoa meupe mbawani. Hana mundu. Jicho lina duara ya njano.

Fimbi-mweupe
Von-der-Decken ‘s Hornbill
Tockus deckeni
Huyu ni mweupe chini na shingoni na domo lake jekundu lina ncha ya kijivu.

Fimbi-mweusi
Grey-Hornbill
Tockus nasutus
Huyu ana domo jeusi lenye mraba mweupe pembeni.


Kielelezo Na. 30 Domongazi

Fimbi-njano
Yellow-billed Hornbill
Tockus flavirostris
Huyu ana domo la njano na madoa meupe mbawani.

Fire
Yellow Bishop
Euplectes capensis
Kwechi mwenye manyoya meroro ya njano yaliyoinuka mgongoni.


Kielelezo Na. 31 Domowazi

Firigogo
Sandgrouse
Pteroclididae
Ndege wadogo kama njiwa, wenye madoadoa kama Kwale, waishio nyasini, nyikani.


Kielelezo Na. 32 Dudumizi

Firigogo-mkia
Chestnut-bellied sandgrouse
Pterocles exustus
Ana mkia mrefu, mwembamba, na tumbo kahawia.


Kielelezo Na. 33 Fimbi-kahawia

Firigogo-mweupe
Black-faced sandgrouse
Eremialector decoratus
Ana mraba mpana na mweupe tumboni na uso mweusi.

Firigogo-njano
Yellow-throated Sandgrouse
Eremialector gutturalis
Huyu ana koo la njano.

Fumbwe-mdogo
Paradise Whydah
Steganura paradisaea
Ndege mdogo wa jamii wa chiriku ambaye dume lake lina mkia mrefu kama wa Chekechea. Kichwa, mkia na mbawa ni nyeusi, tumbo na shingo njano na kifua chekundu. Karibu majike ya Fumbwe wote ni kahawia yenye vimraba vyeusijuu na tumbo kijivu.


Kielelezo Na. 34 Firigogo

Fumbwe-mpana
Broad-tailed Paradise Whydah
Steganura orientalis
Huyu mkia wake ni mpana nchani.

Fundichuma
Blacksmith Plover
Hoplopterus armatus
Ndege wa kando ya maziwa, bahari na mbuga za mito wajamii ya Kiluwiluwi mwenye mchanganyiko wa rangi nyeupe na nyeusi; yaani ana madoa makubwa meusi nyuma, tumbo jeusi, na chini ya mkia, kitosi na shingo nyeupe. Ana sauti ‘tik-tik’ kama chuma mbili zinazogongwa.

Furukombe
Osprev
Pandion halietus
Ndege mweusi kidogo wa jamiiya Tai aliyefananana Yowe, lakini mdogo, mwenye kichwa na tumbo la kijivu na mbawa, mkia na kifua chenye madoadoa meusi. Hakai mbali na maji.


Kielelezo Na. 35 Fumbwe-mdogo

Geuzamawe
Turnstone
Arenaria interpres
Chamchanga mfupi na mnene mwenye domo fupi, nene kiasi, lililopindia juu kidogo. Kwa juu ana milia myeusi na ya kikahawia. Kifua chake ni cheusi na miguu ya njano. Hutafuta chakula kwa kupekuapekua.


Kielelezo Na. 36 Fundichuma

Gogonola
Banded Woodpecker
Campethera taeniolaema
Ndege wajamii ya Kigogota anayetoboa miti. Juu ni kijani, kichwa chekundu na tumbo lina miraba maridadi ya mkato ya njano na kijani.


Kielelezo Na. 37 Geuzamawe


Kielelezo Na. 38 Gogonola

Golegole (Kinuka)
Green Wood-hoopoe (Kakelar)
Phoeniculus purpureus
Ndege mkubwa kiasi wa jamii ya Kilimbimsitu mwenye rangi ya kijani-cheusi inayomeremeta, miguu na domo refu jekundu, mkia mrefu wenye miraba myeupe pembeni na doa jeupe begani.

Hunuka.
Gongofutu
Puff-back Shrike
Dryoscopus cubla
Kipwe wa kijivu-chekundu mwenye tumbo jeupe, macho mekundu na manyoya meroro ya kijivu yaliyoinuka kidogo mgongoni.


Kielelezo Na. 39 Golegole

Gongoshaba
Silverbird
Empidornis semipartitus
Jamiiya shore mwenye mgongo wa shaba na tumbo jekundu.

Gowe
Common Go-away
Corythaixoides concolor
Jamaa wa Denge ambaye ni kijivu kote.

Gudegude (Kipwe-asali)
Cuckoo-Shrike
Campephagidae
Kipwe wadogo kijivu, midomo yao haikupinda na mbawa zao zimefungana nchani na kuinuka juu ya mkia. Wote wana macho ya machungwa na midomo kijivu.


Kielelezo Na. 40 Gude-kijivu

Gude-kijivu
Grey Cuckoo-Shrike
Coracina caesia
Huyu ni kijivu kote.

Gude-mweupe
White-breasted Cuckoo Shrike
Coracina pectoralis
Kama Gude-kijivu lakini tumbo lake ni jeupe.

Gude-mweusi
Black Cuckoo Shrike
Camephaga sulphurata
Huyu ni mweusi. Ana doa jekundu penye shina la domo lake.

Hajivale
Goshawk
Melierax / Micronisus
Mwewe wadogo wa kijivu waliofanana na vipanga. Wana tako jeupe, milia na madoadoa tumboni.


Kielelezo Na. 41 Hajivale

Hanjari (Kwembe-mundu)
Scimitarbill
Phinopomastus minor
Kwembe mweusi mwenye mkia mrefu na domo refu kiasi la njano lililopindia chini kama mundu. Mwenzake ana domo jeusi.


Kielelezo Na. 42 Hanjari


Kielelezo Na. 43 Heroe-mdogo

Heroe-mdogo
Lesser Flamingo
Phoeniconaias minor
Ndege mwekundu wa maziwa ya magadi mwenye miguu mirefu sana, shingo refu ambayo wakati wote huonekana imeinamishwa chini na domo fupi na pana, jekundu sana.


Kielelezo Na. 44 Heroe-mkubwa

Heroe-mkubwa
Greater Flamingo
Phoenicopterus ruber
Huyu ni mkubwa, mweupe, mbawa zake nyekundu na mdomo sio mwekundu sana.

Hinabluu
African Pitta
Pitta angolensis
Ndege mnene wa jamii ya Jole na Kipozamataza mwenye mkia na miguu mifupi, tumbo jekundu, matako ya bluu, madoa ya bluu kwenye mbawa, kofia nyeusi kichwani na mraba kahawia juu ya jicho.


Kielelezo Na. 45 Hinabluu

Hondohondo
Hornbill
Bucerotidae
Ndege wakubwa wa msitu na nyika wa rangi mbalimbali; zaidi nyeusijuu na nyeupe chini, wenye midomo mikubwa ambayo baadhi yake ina mundu juu. Wanakula matunda. Wana sauti kubwa “Ho, ho-ho”, hasa wakati wa magharibi wanaporudi kwenye viota.

Hondohondo-mbili
Black and White-casqued Hornbill
Bycanistes subcylindricus
Hondohondo kubwajeusi lenye mundu kijivu mbele na nyuma mweupe.

Hondohondo-moja
Silvery-cheeked Hornbill
Byeanistes brevis
Hondohondo kubwa jeusi lenye domo la kijivu.


Kielelezo Na. 46 Hondohondo

Hondohondo-mweupe
Trumpeter Hornbill
Bycanistes bucinator
Huyu ana tumbo jeupe na mwanya mkubwa mbele ya mundu.

Hua (Mcheki)
Laughing Dove
Streptopetia senegalansis
Njiwa mdogo kijivu mwenye kifua kibuluu-chekundu na koo jeupe lenye madoadoa chini. Analia “ch-cook, cook-ou, ou”. (Tazama Pugi)


Kielelezo Na. 47 Jogoo-mwitu

Jogoo-mwitu (Kwembe-kisunzu, Hudhud)
African Hoopoe
Upupa africana
Kwembe mwekundu mwenye mkia mfupi, mpana na mweusi, mbawa nyeusi zenye miraba mitatu mipana na myeupe ya mkato na kisunzu chekundu chenye manyoya marefu yaliyoachana na kupangika vizuri kwa ngazi, yenye ncha nyeusi. Kama kawaida ya Kwembe domo lake ni refu, jembamba na limepindia kiasi chini.

Jole
Broadbill
Eurylaimidae (Smithornis)
Ndege mdogo na mnene wa jamii ya Katadole mwenye mdomo mfupi na mnene ambao juu ni mweusi na chini mwekundu. Mgongo ni kahawia-kijivu na tumbo kijivu.


Kielelezo Na. 48 Jole

Jore (Kambu)
Roller
Coraciidae
Ndege wakubwa wanene wa rangi mbalimbali waliofanana na Kasuku (Kwalu) lakini wao midomo yao mipana imenyooka badala ya kufanya “ndoana” kama ya Kasuku.

Jurawa
Grey-headed Sparrow
Passer griseus
Shorewanda mkubwa kahawia mwenye kichwa na kifua cha kijivu na doa jeupe begani. Hana milia wala mraba wa jicho.

Kabilu
European Golden Oriole
Oriolus oriolus
Umbia mwenye tumbo jeupe.


Kielelezo Na. 49 Jore

Kahuja
Lemon Dove
Aplopelia Larvata
Tetere mwekundu mwenye uso mweupe, miguu myekundu sana na baka kijani begani. (Tazama Pugi).

Kalamumbili
Pennant-wing Nightjar
Semeiophorus vexillarius
Kipasuasanda mwenye manyoya mawili marefu mkiani yenye ncha nyembamba. (Tazama Rushana)


Kielelezo Na. 50 Jurawa

Kambu-kahawia
Rufous Roller
Coracias naevia
Jore mkubwa wa kikahawia mwenye domo la kijivu, utosi mweupe na kisogo cheupe.

Kanga
Guinea Fowl
Phasianidae
Ndege mkubwa wa nyika anaeliwa mwenye madoa samawati na meupe. Shingoni ana manyoya marefu yenye miraba ya kupendeza myeusi, samawati na myeupe. Sehemu ya juu ya shingo yake haina manyoya. Mmoja ana vinyoya kisogoni na mwenzake ana kofia ya upembe. (Tazama Chepeo, Kicheleko na Kororo)


Kielelezo Na. 51 Kadogo

Kadogo
Little Stint
Calidris minuta
Chamchanga mdogo kuliko wote; juu ni wa kijivu-chekundu chenye milia hafifu na tumbo jeupe.

Kambu-kijivu
Lilac-breasted Roller
Coracias caudata
Huyu ana kifua chekundu na ncha mbili ndefu mkiani.

Kambu-njano
Red (Broad-billed) Roller
Euristomus glaucurus
Jore mwekundu mwenye kingo za mbawa na mkia samawati (bluu) na domo la njano.


Kielelezo Na. 52 Kambu-kijivu

Kapi
Chiff-chaff, Willow Warbler
Phylloscopus trochilus
Jamii ya Kurumbiza na Pepeo anayekaa kwenye miamba ya sehemu zenye maji. Juu ni wa kijivu na chini kimanjano-cheupe.

Kapurapunda
Puffback flycatcher
Batis capensis
Shore mwenye mgongo kijivu, koo jeupe, kifua cheusi na tumbo jeupe. Jike lina koo la kahawia.

Karani (Tamba)
Secretary bird
Sagittarius serpentalis
Ndege mkubwa kijivu mwenye miguu mirefu na mkia mrefu, mwembamba nchani. Kisogoni ana kisunzu cha manyoya membamba ambayo hutembezwa na upepo. Huonekana mbugani akitembea na kupigapiga chini kwa miguu katika harakati za kutafuta nyoka na vidudu. Manyoya ya mkia wake ni kalamu ya kuandikia.


Kielelezo Na. 53 Kambu-njano

Karemberere
Swallow-tailed Bee-eater
Dicrocercus hirundineus
Mtilili wa kijani mwenye koo la njano na mkia wa ncha mbili kama wa Kijumbamshale.

Kasuku
Grey parrot
Psittacus erithacus
Kwalu mkubwa mnene wa kijivu mwenye sehemu ya chini ya mdomo fupi na sehemu ya juu ndefu iliyopindia chini kufanya ndoana. Mkia wake ni mwekundu. Ndege huyu anaweza kumsikiliza mtu akisema na kurudia baadhi ya maneno yake.


Kielelezo Na. 54 Karani

Kasuku-mapenzi-kahawia
Yellow-collared lovebird
Agapornis personata
Huyu ana kichwa cha kahawia na kifua, shingo na bega la njano.

Kasuku-mapenzi-machungwa
Fischer’s Lovebird
Agapornis fischeri
Huyu ana kichwa cha machungwa na tako la bluu. Ni kijani chini ya mbawa.


Kielelezo Na. 55 Kasuku-mapenzi

Kasuku-mapenzi
Love-bird
Agapornis
Kwalu wadogo, nusu ya kasuku, wanaoishi nyikani.

Kasuku-mapenzi-mwekundu
Red-headed lovebird
Agapornis pullaria
Huyu ana kichwa chekundu, tako la bluu na ni mweusi chini ya mbawa.

Katadole
Longclaw
Macronyx croceus
Ndege mkubwa kiasi, kijivu, wa jamii ya Jole mwenye vidole virefu sana, hasa vya nyuma. Walio wengi ni kahawia, njano chini na wana mraba mweusi kifuani.


Kielelezo Na. 56 Katadole

Kengewa
Kestrel
Falcon
Ndege wadogo wa jamii ya Tai. Wengi wana migongo myekundu yenye madoa, ncha ndefu nyeusi za mbawa na macho meupe. Kengewa mkubwa ana miraba mingi myeusi ya kupendeza mwili mzima.

Kereng’ende
Spur-fowl
Pternistis
Kwale wenye viraka vyekundu au vya njano, na hawana manyoya kooni. Kwale halisi wana manyoya kooni.

Kereng’ende-machungwa
Grey-breasted Spurfowl
Pternistis rufopictus
Huyu ana koo la machungwa.

Kereng’ende-mwekundu
Red-necked Spurfowl
Pternistis afer
Huyu ana koo jekundu.

Kereng’ende-njano
Yellow-necked Spurfowl
Pternistis leucoscepus
Huyu ana koo la njano.


Kielelezo Na. 57 Kereng’ende

Kibeti
Pigmy Goose
Nettapus aurilus
Bata bukini mdogo kama Bluupande ambaye ana domo la njano, mgongo wa kijani-cheusi na ubavu mwekundu.

Kibisi
Grebe
Podicipidae
Ndege wa majini waliofanana na Bata lakini hawa midomo yao imechongoka na hawana mikia.


Kielelezo Na. 58 Kibeti

Kibisi-mdogo mwekundu
Little Red Grebe
Poliocephalus ruficollis
Kibisi mdogo sana kijivu anayefanana na Bata lakini hana mkia. Uso wake na koo ni nyekundu.


Kielelezo Na. 59 Kibisi-mdogo mwekundu

Kibisi-mdogo mweusi
Liltle Black Grebe
Proctopus caspicus
Huyu ni mkubwa zaidi na ana kichwa na shingo nyeusi.


Kielelezo Na. 60 Kibisi-mkubwa

Kibisi-mkubwa
Great-crested Grebe
Podiceps cristatus
Huyu ni mkubwa kumkaribia Bata, ana visunzu viwili vyeusi vilivyotokeza nyuma kichwani na manyoya mengi mafupi na mekundu kuzunguka shingo, chini ya kichwa.

Kibubutu
Cisticola
Cisticola (Sylviidae)
Ndege mdogo kama Chiriku wa nyika za miiba, kahawia, mwenye utosi mwekundu. Aina moja inalia “Chaaaaa-chaaaaa” na nyingine “Tsssss, wiptsssss, wip”.


Kielelezo Na. 61 Kicheba-mweupe

Kicheba-mweupe
Northern Brubru
Nilaus afer
Ndege mdogo wa jamii wa Kipwe; kahawia-kijivu juu, chini mweupe, mbavu nyekundu na ana mraba mweupe juu ya jicho na mwingine uliozunguka mbawa kuanzia begani.

Kicheba-mweusi
Black-browed Brubru
Nilaus nigritemporalis
Huyu hana mraba mweupe wa jicho ila ana milia kifuani.

Kicheleko
Vulturine Guinea-fowl
Acryllium vulturinum
Kanga asiye na manyoya kichwani wala shingoni. Manyoya yake ya chini ya shingo ni marefu na yana rangi za kupendeza nyeusi, nyeupe na za bluu.


Kielelezo Na. 62 Kicheleko

Kichonge
African Snipe
Capella nigripennis
Chamchanga mdogo anayelingana na kufanana na Sululu lakini yeye ana domo refu sana najembamba lililonyooka (karibu kulingana na urefu wa mwili wake) na hana duara nyeupe jichoni.


Kielelezo Na. 63 Kichonge

Kidaku
Black Flycatcher
Melaenornis pammelaina
Shore mweusi aliyefanana na Tiva na Totowo, lakini yeye ana macho meusi.


Kielelezo Na. 64 Kidaku

Kigeugeu
Wheatear Oenanthe
Jamii ya Mkesha wenye matako meupe na mraba mweupe juu ya jicho.

Kigogota (King’oto)
Woodpecker
Picidae
Ndege wadogo wenye rangi za kupendeza ambao husikika au kuonekana wakigogota (wakitoboa) miti. Walio wengi wana rangi ya kikahawia chenye madoadoa na kofia nyekundu. Midomo yao imenyooka. Vidole vyao viwili vimeelekea mbele na viwili nyuma. (Tazama Gogonola)


Kielelezo Na. 65 Kigeugeu

Kigoti (Kibwiko, Maki)
Thicknee (Stone-curlew)
Burhinus capensis
Ndege mkubwa kiasi wa kijivu mwenye madoadoa mengi meusi juu, tumbo jeupe na miguu mirefu yenye magoti manene. Amefanana na Kuluwiluwi. Wengi hukanyagwa na magari usiku.

Kiguudau
African Finfoot
Podica senegalensis
Ndege kahawia wa majini aliyefanana na Bata lakini yeye ana mkia mrefu wenye manyoya magumu, mdomo mwekundu uliochongoka na miguu myekundu yenye vidole vilivyoungana kama pezi ya samaki.


Kielelezo Na. 66 Kigoti

Kuguuhina
Redshank
Tringa totanus
Chamchanga mkubwa kahawia-kijivu mwenyetako jeupe na miguu myekundu.

Kijumbamshale
Swallow
Hirundinidae
Ndege mdogo jamii ya Mbayuwayu mwenye mkia wenye ncha mbili nyembamba na ndefu mara mbili kupita za Mbayuwayu. Baadhi yao huishi kwenye madaraja na nyumba. Walio wengi ni kahawia na bluu.

Kijumbamshale-bluu
Mosque Swallow
Hirundo senegalensis
Juu kibuluu cheusi kinachong’ara, tako jekundu na chini kwekundu. Anaishi kwenye misikiti na mahame.


Kielelezo Na. 67 Kiguudau

Kijumbamshale-kitunga
Wiretailed Swallow
Hirundo smithii
Ana kofia nyekundu, tumbo maziwa na ncha nyembamba.

Kijumbamshale-mraba
European Swallow
Hirundo rustica
Ana uso mwekundu na mraba mweusi kifuani.

Kijumbamshale-mwekundu
Red-rumped Swallow
Hirundo daurica
Kamayule wa kibuluu lakini ncha zake ni ndefu.


Kielelezo Na. 68 Kiguuhina

Kijumbamshale-mweupe
Whiteheaded Swallow
Psalidoprocne albiceps
Ana kichwa cheupe.


Kielelezo Na. 69 Kijumbamshale

Kijumbamshale-mweusi
Black Roughwing Swallow
Psalidbprocne Holomelaena
Ana rangi nyeusi inayong’ara na ncha ndefu.

Kikozi
Harrier Circus
Ndege wadogo wa jamii ya Tai wenye mbawa na mikia mirefu ambao hupaa karibu na ardhi na kuchungulia chini upande-upande kwa makini. Yule anayeonekana mara kwa mara ni wa kijivu-samawati juu, tumbo jeupe na ncha za mbawa zake nyeusi. (Tazama Msenga)


Kielelezo Na. 70 Kikucha

Kikucha
Crombeo
Sylvietta brachyura
Ndege mdogo mwenye mkia mfupi sana ulioinuka juu; juu kijivu, koo jeupe na chini mwekundu.

Kilimbimsitu
Woodhoopoe
Phoeniculidae
Ndege wakubwa wa nyika wenye weusi unaomeremeta, mikia mirefu na midomo mirefu. (Tazama Ngegemea).


Kielelezo Na. 71 Kiluwiluwi

Kiluwiluwi
Plover
Charadriidae
Ndege wakubwa kiasi, jamii ya Chamchanga, wa aina na rangi mbalimbali wa kando ya maziwa, bahari na pwani ya mito mikubwa wenye vidole vitatu vinavyoelekea mbele.

Kiluwingozi
Wattled Plover
Afribyx senegalus
Kiluwiluwi mkubwa kahawia mwenye nyama ya njano na nyekundu (wattle) chini ya macho. Ana utosi mweupe na mdomo kahawia wenye ncha nyeusi.

Kinanda-mweusi
Black-headed Weaver
Ploceus cucullatus
Mnaana wa njano; wa kiume ana kichwa cheusi. Wana kelele nyingi wakati wa kujenga viota.


Kielelezo Na. 72 Kiluwingozi

Kinanda-njano
Speke’s Weaver
Ploceus spekei
Huyu kichwa chake ni cha njano juu na mgongo wake una milia-mingi.

Kindoro
Sparrow Lark
Eremopterix leucopareia
Kipozamataza mdogo aliyefanana na Mtolondo lakini yeye ni wa kijivu na ana kitosi chekundu. Uso, koo, bega na kifua ni vyeusi. Domo lake ni fupi na nene na vidole virefu.


Kielelezo Na. 73 Kindoro

Kinegwa
Martin
Riparia
Ni ndege kahawia jamii ya Kijumbamshale na Mbayuwayu lakini huyu ana mkia mfupi usio na ncha mbili.

Kinegwa-kahawia
African Sand Martin
Riparia paludicola
Ana tumbo jeupe.

Kinegwa-mraba
Banded Martin
Riparia cincta
Ana mraba kifuani.

Kinegwa-mwekundu
African Rock Martin
Riparia fuligula
Ni mwekundu na mkia wake una madoa meupe chini.


Kielelezo Na. 74 Kinegwa

Kinepa-mdogo
Litlle Bee-eater
Mellittophagus pusillus
Mtilili mdogo wa kijani juu, chini mwekundu, mwenye koo la njano. (Tazama Mtilili).

Kinepa-mkubwa
White-fronted Bee-eater
Melittophagus bullockoides
Huyu ana koo jekundu na mraba mweupe chini ya jicho.

Kinubi
Piapiac
Ptilostomus afer
Ndege mweusi wajamii ya Kunguru aliyefanara na Hanjari lakini huyu ana domo fupi na mkia mrefu, mwembamba nchani. Ni mdogo kuliko Mwangapwani.


Kielelezo Na. 75 Kinubi

Kiogajivu-kahawia
European Roller
Coracias garrulus
Jore kahawia mwenye tumbo la kibuluu-kijivu na kichwa kahawia-kijivu. (Tazama Jore).

Kiogajivu-mikia
Rackuet-tailed Roller
Coracias spatulata
Huyu ana ncha mbili ndefu mkiani kama Kambu-kijivu lakini zake zimepanuka nchani.

Kipanga
Kite
Elanus / Milvus
Ndege mdogo wajamii ya Tai mwenye mkia wenye ncha mbili. Yule anayeonekana sana ni kahawia kote na ana domo la njano.


Kielelezo Na. 76 Kipanga-kahawia

Kipanga-kahawia
Black Kite
Milvus migrans
Ni Kipanga wa kikahawia kote, mwenye mdomo wa njano. Huonekana sana katika masikani ya watu. Mwenye mdomo mweusi, anatoka Ulaya.

Kiparara (Komba)
African Skimmer
Rynchops flavirostris
Ndege wa majini anayefanana na Membe; juu mweusi, uso na chini kweupe na mbawa zake ndefu kupita mkia. Mdomo wake mrefu na mwekundu una ncha za njano na domo la juu fupi kuliko la chini.


Kielelezo Na. 77 Kiparara

Kipasuasanda
Nightjar
Caprimulgidae
Ndege wadogo wenye kifua kikubwa kilichotokeza na manyoya mawili ya mkia marefu sana. Wana mbawa ndefu, nyembamba nchani, zinazolingana na mkia. Rangi zao ni za madoadoa kama majani yaliyokauka, ambamo hujificha mchana. Wanawinda wadudu usiku. (Tazama Rushana).


Kielelezo Na. 78 Kipila

Kipila
Black Crake
Limnocorax flavirostra
Ndege mdogo mweusi wa matindiga mwenye mdomo wa kijani-njano na miguu myekundu anayefanana na Kuku-ziwa mdogo.


Kielelezo Na. 79 Kipmi

Kipini
Pintail
Anas acuta
Bata mdogo, jamii ya Bluupande lakini huyu hana rangi ya bluu. Ana shingo ndefu, mraba mweupe wa jicho na mkia mrefu kiasi, mwembamba kama pini nchani.

Kipozamataza
Lark
Alaudidae
Ndege wa chini waimbao vizuri wenye midomo mifupi kiasi na minene na kidole cha nyuma kirefu kukaribia cha Katadole. Walio wengi ni wa kikahawia chenye milia na wana mraba wa jicho. (Tazama Kindoro).


Kielelezo Na. 80 Kipululu

Kipululu
Button Quail
Turnix sylvatica
Ndege kahawia wa jamii ya Tomboro, lakini yeye ana vidole vitatu na hana miraba ya shingo.

Kipupwi
Black-shouldered Kite
Elanus caeruleus
Kipanga wa kijivu mwenye tumbojeupe, begajeusi na mkia wa ncha mbili fupi.

Kipwe
Shrike
Laniidae
Ndege wakubwa wa rangi mbalimbali wenye vifua vipana, mikia mirefu na midomo minene yenye ncha zilizopinda kidogo ambao huwinda kwa kutulia penye tawi la kichaka au mti. Wengi wana macho mekundu.


Kielelezo Na. 81 Kipwe

Kipwe-kahawia
Red-backed Shrike
Lanius collurio
Kipwe wa kijivu mwenye mbawa nyekundu, tako jeupe na mkia mweusi. Jamii yake wana kofia na mkia mwekundu.

Kirumbizi
Oriole
Oriolidae
Ndege wakubwa waliofanana na Kipwe, wa njano, wenye midomo ya rangi ya chungwa. Wamefanana pia na Mnaana wengi kwa rangi, lakini Mnaana hawana midomo ya njano. (Tazama Mramba na Umbia).


Kielelezo Na. 82 Kisharifu

Kisharifu
Pigmy Kingfisher
Ispidina picta
Chopoa mdogo samawati juu, chini kahawia, mwenye koo la kijivu na mdomo mwekundu.

Kiseleagofu
Red-breasted Wryneck
Jynx ruficollis
Ni jamii ya Kigogota mwenye rangi nyingi kama za K-ipasuasanda na Kifua chekundu. Manyoya ya mkia wake si magumu.


Kielelezo Na. 83 Kisigajiru

Kisigajiru
Barbet
Capitonidae
Jamii ya Kigogota wenye rangi za kupendeza zenye madoadoa mekundu, meupe, meusi na ya njano na midomo mifupi na minene sana yenye meno kama msumeno.


Kielelezo Na. 84 Kisigi

Kisigi
Kikuyu White-eye
Zosterops kikuyuensis
Shige wa kijani mwenye duara pana nyeupe kuzungukajicho na mraba mpana wa njano utosini.

Kitaroharo
Shikra
A ccipiter badius
Tai mdogo wa kijivujuu mwenye tumbojeupe lenye milia mingi myeupe ya kukata.


Kielelezo Na. 85 Kitengenya

Kitengenya
Kittlitz’s Sand Plover
Charadrius pecuarius
Chamchanga mdogo wa kijivu-cheusi mgongoni mwenye tumbo la rangi ya maziwa na njano. Miguu na midomo yao ni ya kijivu. Wana miraba meupe ya jicho iliyokutana kisogoni.

Kitibwa
Bush Shrike
Laniidae
Kipwe wa kijani juu, chini njano, wenye macho machungwa.

Kitibwa-kijani
Doherly’s Bush Shrike
Telephorus dohertyi
Ana koo jekundu, utosi mwekundu na mraba mweusi wa kifua.


Kielelezo Na. 86 Kitibwa-kofia

Kitibwa-kofia
Black-headed Bush Shrike
Tchagra senegala
Ni Kipwe wa kahawia-njano mgongoni mwenye tumbo la rangi ya maziwa, kofia nyeusi na mraba wa kahawia juu ya jicho.

Kitibwa-mwekundu
Rosy-patched Bush Strike
Rhodophoneus cruentus
Huyu ni kikahawia-chekundu na tako lakejekundu sana.

Kitibwa-njano
Sulphur-breasted Bush Shrike
Chlorophoneus sulfureopectus
Huyu ni wa kijani-njano juu na chini njano.

Kitibwa-nne
Four-colored Bush Shrike
Telephorus guadricolor
Kama yule kijani lakini hana utosi mwekundu.

Kitibwa-tatu
Grey-headed Bush Shrike
Malaconotus blanchoti
Kama yule njano lakini ana kichwa cha kijivu.


Kielelezo Na. 87 Kitororo

Kitororo (Kirukanjia)
Tinker-bird
Pogoniulus
Ndege wadogo sana wa jamii ya Kisigajiru ambao vidole vyao viwili vinaelekea mbele na viwili nyuma kama Kigogota.

Kitororo-mweusi
Golden-rumped Tinker-bird
Pgoniulus bilineatus
Ni mweusi juu na tako la njano.

Kitororo-njano
Green Tinker-bird
Viridibucco leucomystax
Ni wa kijivu-njano na tako la njano.


Kielelezo Na. 88 Kitwitwi-kijivu

Kitwitwi-kijivu
Mountain Wagtail
Motacilla clara
Ni kijivu juu na chini mweupe. Ana mraba mwembamba kifuani.


Kielelezo Na. 89 Kitwitwi-mraba

Kitwitwi-mraba
Pied Wagtail
Motacilla aguimp
Ndege mdogo mweusijuu na chini mweupe mwenye mraba mweupe mbawani, begani najuuyajicho na mraba mweusi kifuani. Wakati wote mkia wake unatikisika juu na chini.

Kivo
Red-billed Quelea
Quelea quelea
Yomboyombi mkubwa wa kijivu-chekundu mwenye milia ya kahawia mgongoni na kiraka cheusi chini ya jicho. Macho na miguu yake ni mekundu.

Kizamiachaza
Oyster-catcher
Haematopus ostralegus
Jamii ya Domojuu lakini yeye ana mbawa nyeusi, mdomo wa rangi ya chungwa na miguu ya zambarau.


Kielelezo Na. 90 Kizamiachaza

Kizamiadagaa
Malachite Kingfisher
Corythornis cristata
Chopoa mdogo azamiae (mvua) samaki ambaye ni samawati juu, mwekundu tumboni na mdomoni na koo jeupe. Ana kisunzu cha samawati chenye madoa meusi.

Kizezele
Dark-capped (Yellow-vented) Bulbul
Pycnonotus xantopygos
Teleka kahawia-kijivu mwenye kisunzu kidogo cheusi, tumbo la rangi ya maziwa, njano chini ya mkia.

Kizole-mwekundu
Splendid Glossy Starling
Lamprocolius Splendidus
Kwezi mkubwa wa kijani-bluu kinachomeremeta mgongoni na tumboni, mkia mwekundu najicho la njano. (Tazama Nakawa).


Kielelezo Na. 91 Kizamiadagaa

Kizole-mweusi
Redwing Starling
Onychognasus morio
Kwezi mkubwa kuliko wote, mweusi, mwenye macho mekundu na mraba mwekundu mbawani.

Koho
Harrier Hawk
Polyboroides typus
Tai mdogo wa kijivu-bluu mgongoni mwenye tumbo lenye milia myeusi na myeupe na kiraka cha njano penye jicho. Mkia wake mweusi umegawanywa kwa mraba mweupe.

Komakanga-mwekundu
Chestnut Weaver
Ploceus rubiginosus
Ni Mnaana pekee ambaye ni mwekundu. Ana kichwa cheusi, jicho la njano na mdomo na miguu ya kijivu.


Kielelezo Na. 92 Kizezele

Komakanga-njano
Golden-backed Weaver
Ploceus Jacksoni
Kama yule mwekundu lakini ana mgongo wa njano.


Kielelezo Na. 93 Kombe


Kielelezo Na. 94 Kondekonde

Kondekonde
Carmine Bee-eater
Merops nubicus
Ndege mwekundu mla wadudu, jamii ya Mtilili, mwenye kichwa kahawia-samawati na mkia mrefu mwekundu ambao manyoya yake ya katikati ni marefu.

Kombe
Namaque Dove
Oena capensis
Njiwa mdo.go, mweusi usoni na kooni, mwenye mkia mrefu kuliko njiwa wengine. Huonekana kwa wingi bondeni Ngorongoro.

Korongo (Koikoi)
Stork
Ciconiidae
Ndege wakubwa wa rangi mbalimbali, wa nyikani, wenye miguu mirefu, vichwa vidogo, midomo mirefu iliyopanuka na shingo zilizonyooka.

Korongo mfuko-shingo (Kongoti)
Marabou Stork
Leptoptilos crumeniferus
Korongo mkubwa kijivu mwenye shingo na kichwa kisicho na manyoya na nyama kubwa (dehedehe) iliyotokeza kama mfuko shingoni.

Korongo-nyangumi
Whale-headed Slork
Balaeniceps rex
Huyu ni kijivu pia. Ana domo kubwa sana la kijivu lililo kama la nyangumi.


Kielelezo Na. 95 Korongo mfuko-shingo


Kielelezo Na. 96 Korongo-nyangumi


Kielelezo Na. 97 Korongo-samawati

Korongo-samawati
White-bellied (Abdim’s) Stork
Sphenorynchus abdimii
Korongo kahawia-kijani mwenye tumbo na matako meupe, miguu na domo jekundu na ngozi samawati kuzunguka jicho.

Korongo-shingo-hariri
Wooly-necked Stork
Dissoura eipiscopus
Korongo kahawia mwenye miguu na domo la kahawia, mkia mweupe na shingo yenye vinyoya vyeupe nyororo kama hariri.


Kielelezo Na. 98 Korongo-shingo-hariri

Korongo uso-mwekundu (domo-njano)
Yellow-biled Stork (Wood-Ibis)
Ibis ibis
Korongo mweupe mwenye uso na miguu myekundu, kingo za mbawa kahawia-kijani na domo refu la njano.

Kororo
Crested Guineafowl
Guttera pucherani
Kanga wa milimani mwenye kisunzu kikubwa cheusi na madoadoa mengi meupe na samawati shingoni.


Kielelezo Na. 99 Korongo uso-mwekundu

Kotwe
White-backed Duck
Thalassornis leuconotus
Bata mkubwa mwenye milia na madoa meusi, kahawia na meupe, doa jeupe mbele ya jicho na matako meupe yaliyofunikwa na mbawa.

Kozi
Falcon
Falco
Tai mdogo kijivu mwenye kichwa na shingo nyekundu na tumbo jeupe lenye au lisilo na milia maridadi myeusi. Mmoja ni mdogo sana (Kozi-mbilikimo, Pigmyfalcon) na mwekundu mgongoni badala ya kichwani.


Kielelezo Na. 100 Kororo


Kielelezo Na. 101 Kotwe

Kubo
Long-tailed Fiscal Shrike
Lanius cabanisi
Kipwe wa jamii ya Barabara lakini Kubo ni mkubwa, na mbawa na mkia wake sio vyeupe. Mkia wake ni mrefu na mpana. (Tazama Kipwe).


Kielelezo na. 102 Kozi

Kuchi (Sikipi)
Stone Patridge
Ptilopachus petrosus
Ndege wa kikahawia-cheusi chenye madoadoa, wa milima ya mawe. Anafanana sana na mtetea mdogo wa Kuku. Ana tumbojeupe, doa la kijivu nyuma ya jicho na mkia mrefu kiasi ambao wakati wote huinuliwa juu.

Kukuziwa (Fulindi)
Moorhen
Gallinula chloropus
Ndege mweusi wa kwenye maziwa na matindiga, aliyefanana na Kuku na Kipila, mwenye miguu ya kijani, miraba mitano myeupe kando ya mbawa, kiraka chekundu usoni na domojekundu lenye ncha ya njano.


Kielelezo Na. 103 Kuchi

Kulasitara
Heron
Ardeidae (Ardea)
Ndege wakubwa wa kijivu-chekundu kiasi, wajamii ya Korongo na Yangeyange, wenye miguu mirefu na shingo ndefu zilizojikunja kama nyoka kufanya herufi “S”. Wote wana midomo ya kijivu isipokuwa Kulasitara-kijivu ambaye domo lake ni la njano kama la Yangeyange.

Kulasitara-kahawia
Squacco Heron
Ardeola ralloides
Huyu ni mdogo wa kikahawia-njano, mwenye shingo ya kawaida na miguu ya njano.

Kulasitara-kijivu
Night Heron
Nycticorax nycticorax
Umbo lake kama la Kulasitara-kahawia lakini yeye ni kijani-cheusi juu na macho yake mekundu.


Kielelezo Na. 104 Kukuziwa

Kulasitara-kijivu
Grey Heron
Ardea cinerea
Huyu ni wa kijivu. Ana miguu ya njano na pekee mwenye domo la njano. Shingo yake ni nyeupe.

Kulasitara-mwekundu
Goliath Heron
Ardea Goliath
Huyu ni mkubwa, mwekundu na pekee mwenye kisunzu chekundu.


Kielelezo Na. 105 Kulasitara – kijivu

Kulasitara-mweusi
Black-headed Heron
Ardea melanocephala
Huyu ni mweusi na koo lake jeupe.


Kielelezo Na. 106 Kumbakima

Kumbakima
Crowned Hawk-eagle
Stephanoaetus coronatus
Tai mkubwa kahawia mwenye kisunzu kidogo na milia mingi ya mkato tumboni na mkiani.

Kumbamti
African Hawk-eagle
Hieraaetus spilogaster
Tai mkubwa, mweusi mgongoni, mwenye tumbo jeupe, manyoya mengi miguuni na miraba mkiani.

Kunda
Speckled Pigeon
Columba guinea
Njiwa mkubwa, mwekundu juu, mwenye tumbo la kijivu, tako la kijivu-bluu na mbawa zenye madoa meupe.


Kielelezo Na. 107 Kunguru

Kunguru
Pied-Crow
Corvus albus
Ndege mkubwa mweusi jamii ya Mwangapwani mwenye shingo na tumbo jeupe apendaye kukaa karibu na watu. Huonekana kwa wingi kunakotupwa taka. Akichinjwa anatoa matone kama matatu tu ya damu kwa hiyo husemekana hana damu.


Kielelezo Na. 108 Kunguru-mweusi

Kunguru-mweusi (mwoga)
White-naped Raven
Corvus albicollis
Kunguru mkubwa mweusi mwenye shingo nyeupe.

Kung’wani (Sile)
Jacana (Lilly-trotter)
Actophilornis africanus
Kukuziwa mwekundu mwenye koo jeupe, mdomo na kiraka cha uso samawati-kijivu na miguu yenye vidole virefu sana. Kung’wani mdogo (Little-Jacana, Microparra capensis), hana kiraka cha uso, na rangi yake imefifia.

Kungwi
Spotted Eagle-Owl
Bubo africanus
Bundi mkubwa kumkaribia Babewana. Ana rangi ya kikahawia, madoa na miraba mingi myeupe na ya kijivu na macho ya njano. Anapendelea miamba na nyika. Wengi huuawa na magari usiku.


Kielelezo Na. 109 Kung’wani

Kurea-miraba
Striped Kingfisher
Halcyon chelicuti
Chopoa mkubwa kiasi wa kikahawia-kijivu mwenye kichwa cheusi, tako la kijani, koo jeupe na milia meusi. Ana miguu myekundu kama Kurea-mwekundu.

Kurea-mwekundu
Grey-headed Kingfisher
Halcyon leucocephala
Chopoa mkubwa mwenye domo jekundu, kichwa cha kijivu na tumbojekundu. Mkia na mbawa zake ni bluu.


Kielelezo Na. 110 Kurumbiza

Kurumbiza (Papura)
Robin Chal
Cossypha caffra
Ndege mdogo kahawia wa vichaka mwenye mraba mweupe jichoni, tumbo jeupe, koo la kahawia na mraba mweusi mkiani.

Kuruwiji
Sombre Bulbul
Andropadus insularis
Ndege mdogo wa jamii ya Shore-kishungi anayeonekana sana mitini, mashambani na karibu na nyumba. Ni kahawia-kijivu mgongoni, mweusi kichwani, tumbo la njano na kifua kiiivu.


Kielelezo Na. 111 Kuyu

Kuyu
White-Stork
Ciconia ciconia
Korongo mweupe mwenye sehemu za nyuma za mbawa nyeusi na miguu na domo jekundu.

Kuzumburu
Speckled Mouse-bird
Colius striatus
Pwaju kahawia-kijivu mwenye mkia mrefu na mwembamba nchani, madoa ya shingoni na kisunzu. (Tazama Pugi).


Kielelezo Na. 112 Kwale

Kwale (Buwe)
Francolm
Francolinus
Ndege wakubwa wa jamii ya Kuku na jamii ya Kereng’ende, wenye nyama tamu. Karibu wote wana milia na madoa mwilini na kipia mguuni. Wachache wana koo au miguu ya njano au myekundu. Wanatofautishwa na Kereng’ende kwa koo zao zenye manyoya.

Kwale-koojeupe
Jackson’s Francolin
Francolinus jacksoni
Huyu ana miguu na domo jekundu na koo jeupe.

Kwale-miguunjano
Coqui Francolin
Francolinus coqui
Huyu’ana miguu ya njano.

Kwale-mwekundu
Hildebrandt ‘s Francolin
Francolinus hildebrandti
Huyu ana miguu na domo jekundu.

Kwale-njano
Ring-necked Francolin
Francolinus streptophorus
Huyu ana miguu na tumbo la njano na domo la kijivu.


Kielelezo Na. 113 Kwalu

Korongo wadogo wasio na miguu mirefu sana ambao midomo yao imepindia chini na shingo zao zimepinda kidogo kama za Kulasitara.

Kwarara-kijani
Hadada Ibis
Hagedashia hagedash
Kwarara wa kijani-kijivu mwenye miguu myekundu, mbawa za kijani na domo kahawia.

Kwarara-kishungi
Green Ibis
Lampribis olivacea
Kama yule kijani lakini ana kishungi.

Kwarara-mwekundu
Glossy Ibis
Plegadis falcinellus
Kwarara mwekundu mwenye miguu ya kikahawia-njano, sehemu ya chini na nyuma ya mbawa ya kijani na domo refu jembamba la kijivu.

Kwarara Shingo-nyeusi
Sacred Ibis
Threskiornis aethiopicus
Kwarara mweupe mwenye miguu na shingo nyeusi, domo la kijivu na manyoya meusi meroro juu ya mkia.

Kwaru-mwekundu
Red-headed Weaver
Anaplectes melanotis
Mnaana kahawia mwenye domo na kichwa

Kwalu
Parrot
Psittacidae
Aina mbalimbali za jamii ya Kasuku.

Kwalu-kijani
Red-headed Parrot
Poicephalus gulielmi
Huyu ni kijani kote isipokuwa utosi wake ambao ni mwekundu na ana mraba mwekundu mbawani.

Kwalu-inachungwa
Orange-bellied Parrot
Poicephalus rufiventris
Huyu ni kahawia-kijivu juu, tumbo la machungwa na macho mekundu.

Kwalu-kahawia
Brown-headed Parrot
Poicephalus cryptoxanthus
Kwalu mkubwa wa kijani mwenye kichwa cha kahawia-kijivu. Anapendelea sana vichaka vya pwani.

Kwalu-utosinjano
Brown Parrot
Poicephalus meyeri
Huyu ni kahawia-kijivu juu, tumbo kijani na utosi wa njano.

Kwarara (Haha)
Ibis
Threskiornithidae
chekundu na kiraka cheusi chini ya jicho. Amefanana kidogo na Kivo lakini Kwaru ni mkubwa zaidi na tumbo lake ni jeupe.


Kielelezo Na. 114 Kwarara shingo-nyeusi

Kwaru-mweupe
Grey-headed Weaver
Pseudonigrita arnaudi
Huyu ni kahawia kote na kichwa cheupe.

Kweche (Bombo)
Bishop
Euplectes
Ndege weusi wenye midomo mipana ya kijivu wa jamii ya Chekechea ambao wana rangi nyekundu au ya njano kichwani, mbawani au matakoni.

Kweche-machungwa
Black Bishop
Euplectes gierowii
Huyu ni mweusi na ana kisogo, tako, bega na mraba wa machungwa kufuani.

Kweche-mraba
Red Bishop
Euplectes oryx
Huyu ni mwekundu juu na kifuani; tumbo na uso mweusi.

Kweche-mwekundu
Zanzibar Red Bishop
Euplectes nigroventris
Huyu ni mwekundujuu na chini mweusi. Ni mdogo.


Kielelezo Na. 115 Kweche-mweusi

Kweche-mweusi
Blackwing Bishop
Euplectes hordeacea
Huyu ni mweusi. Ana kichwa na tako jekundu na kiraka cheusi chini ya jicho.

Kwezi
Starling
Sturnidae
Ndege wakubwa kama Kwembe wenye rangi mbalimbali maridadi kama Chozi. Walio wengi ni kijani-samawati na machungwa na wana midomo ya kijivu. Wanapenda kuishi mashambani.

Kwezi-bluu
Blue-eared Glossy Starling
Lamprocolius chalybaeus
Huyu ni kijani-biuu kote. Ana jicho la njano lililozungukwa na kiraka cha bluu sana.

Kwezi-dehe
Wattled Starling
Creatophora Cinerea
Ana dehedehe (ngozi) refu kooni na kiraka cha njano nyuma ya jicho.


Kielelezo Na. 116 Kwezi-njano

Kwezi-njano
Golden-breasted Starling
Cosmopsarus regius
Ana tumbo la njano na macho meupe.

Kwezi-zambarau
Violet-backed Starling
Ginnyricinclus leucogaster
Ana rangi ya zambarau juu na tumbo jeupe.


Kielelezo Na. 117 Levi

Levi (Magamaga)
Prinia
Prinia subflava
Ndege kahawia, jamii ya Pepeo, mwenye mkia unaoelekezwa juu, mbawa fupi zinazoelekea chini na mraba wa kijivu jichoni. Mwendo wake ni wa kupepesuka kama mlevi.


Kielelezo na. 118 Macho-kioo

Machokioo
Camaroptera
Camaroptera
Pepeo mdogo wa kijani-kijivu mwenye mkia na mbawa kamaza Levi. Macho yake yanang’ara kama kioo.


Kielelezo Na 119, Madende

Madende
Morning Warbler
Cichladusa guttata
Jamii ya Mkesha mwenye mkia mpana mwekundu unaoelckezwa juu. Tumbo lake jeupe lina madoa marefu yaliyopangika vizuri katika mistari.

Malenga
Singing Cisticola
Cisticola cantans
Huyu ni yule Kibubutu wa kikahawia-kijivu mwenye kofia nyekundu na tumbo la rangi ya maziwa ndege huyu huimba vizuri sana.

Mangisi
White-headed vulture
Trigonoceps occipitalis
Tumbusi kahawia mwenye kichwa cheupe na domo jekundu.

Manja
Yellow White-eye
Zosterops senegalensis
Shinge wa njano mwenye duara nyeupe nyembamba kuzunguka jicho na mraba mdogo wanjanoutosini. (Tazama Kisigi)

Manofi
White-headed Buffalo Weaver
Dinemellia dinemelli
Mnaana mkubwa kahawia-kijivu mwenye domo pana; mbele na kichwani mweupe, na takojekundu.


Kielelezo Na. 120 Manofi

Marumbi
Lanner
Falco biarmicus
Jamii ya Tembere, ambaye wamefanana kwa mbawa zao nyembamba isipokuwa marumbi ana kisogo chekundu.

Mata-kijivu
Nyanza Swift
Apus niansae
Mbayuwayu wa kijivu-cheusi mwenye koojeupe na mkia wenye ncha mbili ndefu kukaribia za Kijumbamshale. Mbawa zake ni nyembamba na ndefu.

Mata-mweupe
Horus Swift
Apus horus
Ana tako jeupe.


Kielelezo Na. 121 Marumbi

Matepe
Long-crested hawk-eagle
Lophoaetus occipitalis
Tai mkubwa kiasi, mweusi, mwenye kishungi kirefu na doa refu jeupe mbawani.

Mbayuwayu
Swift
Apodidae
Ndege wadogo jamii ya, na waliofanana na Kijumbamshaie wenye mbawa zilizokaa kama upinde na mikia yenye tawi mbili ndetu kiasi, Wana mbio sana.

Mbayuwayu-kijivu
Palm Swift
Cypsiurus parvus
Huyu ni wa kijani-kijivu kote na ncha za mkia wake ni ndefu na nyembamba. Anapendelea minazi na mikoche.


Kielelezo Na. 122 Mbayuwayu-mweupe

Mbayuwayu-mweupe
White-rumped Swift
Apus caffer
Huyu ana koo na tako jeupe. Ncha zake ni ndefu kuliko za Mata lakini hazifikii za mwenzake Mbayuwayu-kijivu.

Mbizi
African Darter
Anhinga rufa
Ndege mweusi wa majini mwenye shingo nyekundu iliyopinda kama ya nyoka (na Kulasitara) yenye mraba mwekundu wa kuteremka.


Kielelezo Na. 123 Mbizi

Mbuni
Ostrich
Struthio camelus
Ndege mkubwa kuliko wote hapa duniani (urefu 8′, 250 cm) asiyeruka; pekee mwenye vidole viwili mguuni. Juu ni mweusi na chini mweupe. Jike ni kijivu juu. Mayai yake makubwa.


Kieielezo Na. 124 Mbuni

Mchungi (Fuata-ng’ombe)
Cattle Egret (Buff-backed heron)
Bubulcus ibis

Yangeyange mdogo wa njano kiasi mwenye miguu na domo la njano ambae hufuatana na ng’ombe na Mbogo.

Mdiria-kijani
Narina Trogon
Apaloderma narina
Ndege mkubwa kama Kunguru wa kijani cheusi kinachong’aa juu na kufuani, tumbo jekundu, mdomo mfupi, mpana sana wa njano najichojeusi.


Kielelezo Na. 125 Mdiria

Mdiria-miraba
Bar-tailed Trogon
Heterolrogon vittatum
Huyu ana miraba myeusi na myeupe kandokando ya mkia na macho ya machungwa.


Kielelezo Na. 126 Membe-mweupe

Membe-mweupe
Gull-billed Tern
Gelochelidon nilotica
Ndege kijivu wa majini aliyefanana na Shakwe (gull) mwenye domo na kichwa cheusi. Mkia wa huyu umegawanyika kidogo kama wa Mbayuwayu wakati wa Shakwe ni mzima.


Kielelezo Na. 127 Membe-mweusi

Membe-mweusi
White-winged Black Tern
Chlidonias leucoptera
Huyu ni mdogo na mweusi isipokuwa mbawa zake ni nyeupe.

Membe-njano
Crested Tern
Sterna bengalensis
Kama yule mweupe lakini domo lake njano.


Kielelezo Na. 128 Mguu-kijani

Mguu-kijani
Greenshank
Tringa nebularia
Chamchanga mkubwa wa kijivu mwenye fumbo na tako jeupe, na miguu ya kijani.

Mkesha
Thrush
Turdidae
Ndege wa jamii ya Kurumbiza; juu kahawia-kijivu, tumbo jekundu na miguu na domo njano. Wengine wana madoa kifuani. (Tazama Chiru).


Kielelezo Na. 129 Mkumburu

Mkumburu
Giant King-fisher
Megaceryle maxima
Chopoa mkubwa kuliko wote. Kichwa chake kina kishungi kikubwa cheusi, mgongo na mkia ni kijani- kijivu chenye madoadoa meupe, shingo nyeupe, tumbo jeupe lenye milia na kifua chekundu.


Kielelezo Na. 130 Mlamba-ncha

Mlamba-ncha (Mabangi)
Fork-tailed Drongo
Dierurus adsimilis
Ndege mkubwa kama Kipwe, mweusi, mwenye mkia mrefu ulio kama wa samaki na macho mekundu. Mkia wa Kipwe mweusi, ambaye wamefanana, hauna pengo. Shore-kishungi mweusi ni mdogo na mkia wake hauna pengo.

Mlamba-sawiya
Square-tailed Drongo
Dierurus Ludwigii
Huyu ni mdogo na mkia wake hauna ncha mbili.

Mleli-mikia
Long-tailed Widow-bird
Coliuspasser progne
Chekechea mkubwa mweusi mwenye mkia mrefu sana na doa jekundu penye ubawa.

Mleti-mwekundu
Red-collared Widow -bird
Coliuspasser ardens
Huyu ana kisogo na kifua chekundu na mkia mrefu, mwembamba kiasi.


Kielelezo Na. 131 Mleli-mweusi

Mleli-mweusi
Jackson’s Widow-bird
Drepanoplectes jacksoni
Huyu ana domo pana sana na mkia mrefu uliopanuka chini.

Mlemba
Cuckoo
Cuculidae
Ndege wakubwa wa jamii ya, na waliofanana na, Dudumizi na Kipwe. Wanatofautishwa na Kipwe kwa mikia yao mirefu na mipana na midomo yao ya njanonjano. (Tazama Semkoko)


Kielelezo Na. 132 Mlembe

Mlembe (Kiongozi-asali)
Honey Guide
Indicatoridae
Ndege wadogo wanaofanana na Shore-kishungi ambao hula mazana (masega) na watoto wa nyuki. Manyoya ya pembeni ya mikia yao ni meupe. Yule anayeongoza watu na Nyegere kwenye mizinga ana koo jeusi na domo la kikahawia. Akikuongoza kwenye asali usipompa, safari nyingine atakuongoza kwenye hatari.


Kielelezo Na. 133 Mlimi-kahawia

Mlimi-kahawia (Kanghagha)
Rufous Chatterer
Argya rubiginosa
Ndege mkubwa kama Shorekishungi mwenye wekundu uliofifia mgongoni, domo na macho ya njano na kelele nyingi sana.

Mlimi-kijivu
Scaly Chatterer
Argya aylmeri
Huyu ni wa kijivu chenye milia kahawia kooni na kichwa kahawia. Njano ya domo lake imefifia.


Kielelezo Na. 134 Mlonjo

Mlonjo
Black-winged Stilt
Himantopus himantopus
Ndege mkubwa kama Domo-juu wa kando ya maziwa, mwenye domo refu jembamba na jeusi lililonyooka, kichwa na tumbo nyeupe, mbawa nyeusi na miguu mirefu sana, myekundu.

Mluli
White-throated Bee-eater
Aerops albicollis
Mtilili wa kijani-kijivu mwenye koojeupe na msitari mweupe juu ya jicho.

Mnaana
Weaver
Ploceus (Ploceidae)
Ndege wakubwa kiasi wanaojenga viota mviringo kwa wingi pamoja, wengi ni kijani-njano juu na njano chini na wachache wekundu na weusi. Wana midomo ya kijivu. Wakati wa kujenga viota wana makelele mengi.


Kielelezo Na. 135 Mnaana

Mnandi (Luvuvi)
Cormorant
Phalacrocoracidae
Ndege weusi wa majini waliofanana na Bata lakini hawa wana mikia mirefu (ya kawaida ya ndege) na shingo ndefu kiasi zilizokaa kama za Kulasitara.

Mnandi mkia-mrefu
Long-tailed Cormorant (Peed Duiker)
Phalacrocorax africanus
Ndege mweusi wa kando ya maji mwenye mkia mrefu na shingo iliyopinda kidogo kama ya mbizi.


Kielelezo Na. 136 Mnandi shingo-nyeupe

Mnandi shingo-nyeupe
White-necked cormorant
Phalacrocorax carbo
Huyu ni mkubwa zaidi na shingo yake nyeupe. Kafanana sana na Mbizi lakini Mbizi ana shingo nyekundu na ina mraba.

Mnekeuta (Sumeno)
Double-toothed Barbet
Lybius bidentatus
Ndege mkubwa kama Kwalu (Kasuku) wajamii ya Kigogota; juu ni mweusi, mbele mwekundu, domo kubwa jeupe lenye meno (visumeno) mawili na ana doa jeupe takoni na juu ya mguu. Jicho lake limezungukwa na duara ya njano. (Tazama Kisigajiru).

Mpayupayu-milia
Arrow-marked Rabbler
Turdoides jardirei
Ndege mkubwa kama Shorekishungi; kahawia-kijivu juu, mweupe kooni na macho ya njano, mwenye kuishi katika makundi makubwa yenye kelele. Ana milia myeupe kifuani na mabegani.


Kielelezo Na. 137 Mpayupayu-milia

Mpavupayu-mweusi
Pied Babbler
Turdoides hypoleuca
Huyu ni wa kikahawia cheusijuu na chini mweupe.

Msasi
Tawny Eagle
Aquila rapax
Tai mkubwa kama Kumbamti lakini huyu ni kahawia mwili mzima, na ndiye pekee mwenye mbawa zilizolingana na mkia. Ana manyoya miguuni na sauti kubwa kama ya Cheusi.

Mramba
Black-headed Oriole
Oriolus larvatus
Kirumbizi wa njano mwenyekichwacheusi nadomo la machungwa. Kafananana Mnaana-kichwacheusi lakini Mnaana hawana midomo ya machungwa.


Kielelezo Na. 138 Mramba

Msenga
Pallid harrier
Circus macrourus
Kikozi mdogo wa kijivu mgongoni mwenye tumbo jeupe na ncha za mbawa nyeusi.

Msese
Whydah-bird
Vidua
Wala nafaka waliofanana na Chiriku, jamii ya Fumbwe, wenye mikia mirefu sana na myembamba.

Msese-mweusi
Pintailed Whydah
Vidua microura
Huyu ana mkia mweusi na kofia nyeusi.

Msese-njano
Straw-tailed Whydah
Vidua fischeri
Huyu ana mkia wa njano na kofia ya njano.


Kielelezo Na. 139 Msese


Kielelezo Na. 140 Msese-mweusi

Mshigi-mwekundu
Waxbill
Estrilda astrild
Chiriku mdogo wa kikahawia-kijani mwenye tumbo na domo jekundu, mraba mwekundu jichoni na tako kahawia. Mwenzake ana tako jekundu.


Kielelezo Na. 141 Msese-njano

Mshigi-njano
Yellow-bellied Waxbill
Cocopygia melanotis
Huyu ana domo la juu jeusi, la chini jekundu na tumbo la njano.

Mshingi (Mnguri, Nyundo)
Hammerkop
Scopus umbreta
Korongo mdogo kahawia mwenye nyundo kisogoni.


Kielelezo Na. 142 Mshigi-njano

Msilimiwa
Brimstone Canary
Serinus sulphuratus
Chiriku wa kijani-njano mgongoni. Hana utosi wa njano kama jamii yake Chingi.


Kielelezo Na. 143 Mshingi

Mtama-wa-Bibi (Domofupi)
White-breasted Tit
Paridae
Ndege wadogo kama Mtolondo wenye vidomo vidogo sana, vyembamba nchani. Mikia yao ni mifupi kiasi na huelekezwa nyuma. Wana tumbo jeupe na vifua vyeusi au vya kijivu. Mmoja, anayeonekana zaidi, ni yule mweusi mwenye tumbo jeupe na kiraka cheupe kati ya mbawa.


Kielelezo Na. 144 Msilimiwa


Kielelezo Na. 145 Mtama-wa-bibi

Mtilili
Bee-eater
Meropidae
Ndege wenye rangi za kupendeza, midomo myembamba na mirefu, macho mekundu na nyoya za katikati ya mkia ndefu. Hula wadudu.

Mtiti
Owlet
Glaucidium
Bundi wadogowasio na manyoya kwenye masikio. Wana mikia miretu kuliko wenzao na macho yao ni ya njano.


Kielelezo Na. 146 Mtilili

Mtolondo
Red-billed Fire Finch
Lagonosticta senegala
Chiriku wadogo wekundu (juu kahawia kidogo) wenye midomo myekundu wanaopenda sana kutembeatembea nje ya nyumba; mara kwa mara wakiwa wamefuatana na Kwezi.


Kielelezo Na. 147 Mtolondo

Mtolondo-kanga
Twin Spot
Hypagos (Mandingoa)
Mshingi mrembo mwenye madoa makubwa meupe tumboni.


Kielelezo Na. 148 Mtolondo-kanga

Mumbi
Ground Hornbill
Bucorvus leadbeateri
Hondohondo mkubwa mweusi anayetembea chini mwenye uso na koo jekundu; kafanana na Bata-mzinga (Turkey). (Watu wengi wanaamini kuwa ukimuua utakufa lakini sio kweli).

Mwanjiko
Magpie-Shrike
Urolestes melanoleucus
Kipwe mkubwa kuliko wenzake, mweusi, mwenye tako jeupe, “V” nyeupe mgongoni na mkia mrefu sana.

Mwangapwani
Cape Rook
Corvus capensis
Kunguru mkubwa mweusi mwenye ndevu ambaye huonekana zaidi pwani


Kielelezo Na. 149 Mumbi

Mwari
Pelican
Pelecanidae
Ndege wakubwa wa kijivu wa majini waliofanana na Korongo wenye midomo mirefu yenye upanga chini. Wana kishungi kidogo kisogoni na ncha nyeusi mbawani.

Mwari-mwekundu
Pink-backed Pelican
Pelecanus rufescens
Mwari wa kijivu mwenye takojekundu na kishungi kisogoni.

Mwari-mweupe
White Pelican
Pelecanus onocrotalus
Mwari mweupe mwenye kishungi kidogo sana na, kama mwenzake, mbawa zenye kingo nyeusi.

Mwenge-bluu
Violet-crested Turaco
Gallirex porphyreolophus
kama Mwenge-kijani huyu kitunga chake ni cha bluu. (Tazama Shorobo).


Kielelezo Na. 150 Mwangapwani

Mwenge-kijani
Livingstone’s Turaco
Turaco Livingstonii
Dura wa kijani aishiye kwenye misitu na nyika. Ana manyoya marefu ya kijani yenye ncha nyeupe kichwani, domo jekundu, duara nyekundu kando ya jicho na mraba mwekundu mbawani. (Tazama Shorobo).


Kielelezo Na. 151 Mwari-mweupe

Mwewe
Hawk
Accipiter
JamiiyaTai nawakubwa kuwakaribia. Wengijuu ni weusi na chini weupe. Wanashambulia sana kuku.

Mwigo
Red-eyed Dove
Streptopelia semitorquata
Njiwa wa kijivu mwenye mraba mweusi shingoni, tumbo la kahawia na jicho jekundu. Huonekana mara kwa mara (Iazama Pugi)

Mwimbizi (Mleke)
African Hobby
Falco cuvier
Tai mdogo wa kijivu-cheusi juu mwenye tumbo jekundu lenye milia michache ya kuteremka na koo jeupe.

Nakawa-mwekundu
Hildebrandt’s Starling
Sprea hildebrandti
Kama yule mweupe lakini hana mraba. Ana jicho jekundu.


Kielelezo Na. 152 Nakawa-mweupe

Nakawa-mweupe
Superb Starling
Spreo superbus
Kwezi mkubwa kiasi, mrembo, mwenye mgongo na kifua cha samawati, tumbo la kikahawia-chekundu lenye mraba mweupe, manyoya meupe chini ya mkia na jicho la rangi ya maziwa.

Neli-kijani
Malachite sunbird
Nectarinia johnstoni
Chozi kijani wa milimani mwenye mkia mrefu.

Neli-mwekundu
Golden-winged sunbird
Nectarinia reichenowi
Huyu ni mwekundu kote.


Kielelezo Na. 153 Neli-mwekundu

Ndoero
Long-toed lapwing
hemiparra crassirostris
Kiluwiluwi mkubwa mwenye uso, shingo natumbo jeupe, kifua na kisogo cheusi, domo jekundu lenye ncha nyeusi na miguu myekundu yenye vidole virefu. Hupendelea majani yanayoelea majini kama Kung’wani.

Nenda
Bare-faced Go-away
Gymnscnizorhis personata
Jamii ya Denge ambaye ni wa kijivu. Ana kifua na shingo nyeupe na uso mweusi usio na manyoya.

Ngegemea
White-headed Woodhoopoe
Phoeniculus bollie
Kilimbimsitu mweusi mwenye kichwa cheupe.


Kielelezo Na. 154 Ndoero

Ngojamaliko
Little Bittern
Ixobrychus minutus
Kulasitara mdogo wa kijani-kijivu mwenye milia midogo myeupe na shingo nyekundu.

Nguo (Kipwe-hina)
Gonolek
Laniarius erythrogaster
Kipwe wa vichaka ambaye ni ndege pekee mweusi tititi juu na mwekundu tototo chini.

Ngusha
Nubian (lappet-faced) Vulture
Targos tracheliotus
Tumbusi mkubwa kuliko wote mwenye kichwa na domo kubwa, manyoya ya shingo yaliyoinuka na kisogo chekundu na zambarua kilichokunjamana.


Kielelezo Na. 155 Nenda

Nili
Indigo (Purple) – bird
Hypochera ultramarina
Ndege kijani na zambarau jamii ya msese na Fumbwe


Kielelezo Na. 156 Ngegemea

Ninga
Green Pigeon
Treron australis
Njiwa wa kijani mwenye miguu myekundu. (Tazama Pugi)


Kielelezo Na. 157 Ngojamaliko

Njiwa
Olive Pigeon
Columba arquatrix
Ndege mkubwa kiasi na mnene aliyefanana na Kasuku; kahawia mgongoni, tumbo la kijivu-chekundu chenye madoa meupe, na mdomo na miguu ya njano. Mwenzake ana madoa mbawani na miguu na domo la kijivu. (Tazama Pugi)

Nyangala (Kizole)
Black-breasted Starling
Lamprocolius corruscus
Kizole mwenye kifua cheusi, wa Pwani na Unguja. (Tazama Nakawa).

Pasha-kishungi
Crested Malimbe
Malimbus
Chekechea mweusi mwenye kichwa na kifua chekundu.


Kielelezo Na. 158 Pasha-kitunga

Pasha-kitunga
Red-headed Malimbe
Malimbus
Huyu kifua chake ni cheusi.

Pasuambegu (Gawa)
Streaky Seed-eater
Serinus striolatus
Chiriku kahawia mwenye milia ya kijivu ya kuteremka na mraba mweupe juu ya jicho. Huonekana sana mashambani, sehemu za milimani.

Pembenvekundu (Nyuni)
Red-knobbed Coct
Fulica cristara
Jamii ya Kukuziwa, lakini mkubwa zaidi na mweusi, mwenye domo jeupe na virungu viwili vyekundu usoni.

Pepeo
Warbler
Sylviidae
Ndege kahawia-kijivu wanaofanana na Shore-kishungi, wanaorukaruka chini vichakani. Mkao wao ni wa kusimama na mikia ya kawaida. Baadhi yao hutikisatikisa mikia kama Kitwitwi. (Tazama Madende).


Kielelezo Na. 159 Pasuambegu


Kielelezo Na. 160 Pembenyekundu

Pigile (Kobwe)
Lapwing (Crowned Plover)
Stephanibyx coronatus
Kiluwiluwi wa kikahawia-kijivu mwenye kofia nyeusi iliyozungukwa na msitari mweupe, miguu myekundu na domo jekundu lenye ncha nyeusi. Hupiga mbawa zake “lap, lap”.

Polisi
Brown Bohby
Sula Leucogaster
Ndege wa majini wa kikahawia-kijivu juu na chini weupe, wenye miguu ya njano na waliofanana na Kibisi-mdogo.

Polohoyo
European Bee-eater
Merops apiaster
Mtilili wa kikahawia-kijivu mwenye tumbo la samawati na sHngo ya njano.


Kielelezo Na. 161 Pigile

Pugi
Rmg-necked Dove
Streptopelia capicola
Njiwa kahawia mwenye mraba mweusi shingoni kama Mwigo lakini tumbo lake ni jeupe, na ni mdogo.

Pungu
Bateleur Eagle
Terathopius ecaudatus
Tai mnene kahawia mwenye mkia mfupi sana wa kahawia uliopitwa na mbawa, kichwa kikubwa cheusi na doa panajeusi sehemu yajuu ya mbawa.

Pwaiu
Mousebird
Collidae
Ndege kahawia-kijivu jamii ya Mlembe (Kiongozi – asali) mwenye kisunzu na mkia mwembamba, mrefu. Mmoja ana madoa kooni.


Kielelezo Na. 162 Pugi

Pwaju-bluu
Blue-naped Mousebird
Colius macrourus
Huyu ana kisogo cha bluu.

Pwaju-mwekundu
Red-faced Mousebird
Colius indicus
Huyu ana duara pana nyekundu kuzunguka jicho.

Rega
Yellow-rumped Canary
Serinus astrogularis
Chiriku mdogo wa kimanjano-kijivu juu na chini maziwa mwenye tako la njano.


Kielelezo Na. 163 Pungu

Rushana
Standard-wing Nightjar
Macrodipteryx longipennis
Kipasuasanda mwenye mishale miwili mirefu sana nyuma ya mkia ambayo mwishoni imepanuka na kuwa kama fimbo ya kuchezea gofu.


Kielelezo Na. 164 Pwaju-bluu

Salili
Cape Wigeon
Anas capensis
Bata mdogo wa kikahawia-kijivu juu mwenye tumbo jeupe na mdomo mwekundu.


Kielelezo Na. 165 Rega

Sautisaba
Whimbrel
Numenius phaeopus
Jamii ya Chekeamwezi lak’ni ni mdogo zaidi na ana mraba kahawia wa mkato kichwani. Kama mwenzake ana domo refu lililopindia chini na sauti yake ina milio saba.

Sekini (Kipwe-visunzu)
Helmet Shrike
Prionopidae
Kipwe wenye manyoya marefu kidogo uso na ngozi ya njano isiyo na vinyoya kuzunguka jicho.

Sekini-mweupe
White-crowned Helmet Shrike
Eurocephalus anguitimens
Ana kichwa, tako na tumbo jeupe na mgongo wa kikahawia-kijivu.


Kielelezo Na. 166 Rushana

Sekini-mweusi
Retz’s Helmet Shrike
Sigmodus retzi
Huyu ni mweusi na ana mbawa za kahawia na macho ya njano yenye duara nyekundu.


Kielelezo Na. 167 Salili


Kielelezo Na. 168 Sautisaba

Semkoko-kahawia
Common Cuckoo
Cuculus canorus
Mlemba kahawia mwenye miraba myeupe ya mkato mkiani na domo na macho ya njano.

Semkoko-mwekundu
Red-chested cuckoo
Cuculus solitarius
Huyu ana kifua chekundu na macho ya machungwa.

Sepeto
European shoveller
Spatula clypeata
Ndege wa majini aliyefanana na Bata mwenye domo lililopanuka kama beleshi nchani. Ana kichwa cheusi, tumbo jekundu, kifua cheupe na mbawa zenye kiraka cha samawati.

Shakivale
Buzzard
Buteo
Tai wakubwa kiasi ambao wakiruka mbawa zao huonekana pana. Mmoja wao (Augur – Shakivale-mwekundu) ana mkia mwekundu.


Kielelezo Na. 169 Semkoko-kahawia

Shakwe
Gull
Larus (Laridae)
Ndege wakubwa kiasi wa kandokandoya maji na walifanana na Kiluwiluwi lakini sehemu zao zajuu ya miguu ni fupi. Vidole vyao vitatu vya mbele vimeungana kama vya Bata, na wana vidole vidogo sana vya nyuma. Wanaishi katika vikundi na wana mlio mkubwa kama wa Yowe.

Shakwe-mweupe
Grey-headed Gull
Larus cirrocephalus
Shakwe kijivu wa maji ya maziwa na mito mwenye kichwa kijivu na tumbo jeupe.


Kielelezo Na. 170 Sepeto

Shakwe-mweusi
Sooty Gull
Larus hemprichii
Shakwe wa kijivu-cheusi mwenye shingo nyeupe na kichwa cheusi. Hupatikana zaidi sehemu za pwani.

Shani
Golden Pipit
Tmetothylacus tenellus
Ni Kipozamataza mdogo wa njano kote mwenye mgongo wa kijani na mraba mweusi kifuani. Akiruka anaonekana njano kama chiriku.

Shaunge-kijani
Allen’s Gallinule
Porphyrula alleni
Kama yule mwekundu lakini huyu ni mdogo na rungu zake ni za kijani.


Kielelezo Na. 171 Shakivale-mweusi

Shaunge-mwekundu
Purple Gallinule
Porphyrula porphyrio
Jamii yake Pembe mwekundu lakini huyu juu ni kijani, kichwa na tumbo kahawia na domo, uso na miguu myekundu.

Shinge
White-eye
Zosteropidae
Jamii ya Pepeo ambayejuu ni kijani, chini njano na ana mviringo mweupe kuzunguka jicho na mraba wa njano kichwani. Hukaa kwa wingi. (Tazama Kisigi na Manja).


Kielelezo Na. 172 Shakwe-mweupe

Shomoro
Sparrow Weaver
Plocepasser mahali
Mnaana mkubwa wa kikahawia juu na chini mweupe, mwenye tako jeupe na mraba mweupe wa jicho. Huishi kwa wingi.


Kielelezo Na. 173 Shakwe-mweusi


Kielelezo Na. 174 Shaunge-mwekundu

Shongo
Red-fronted Tinkerbird
Pogoniulus pusillus
Kitororo mwenye utosi mwekundu na madoadoa mgongoni.

Shore (Ndwindwi)
Fly-catcher
Muscicapidae
Jamii ya Chole na Teleka wenye masharubu. Baadhi yao wana mikia mirefu kama ya Pwaju lakini mipana zaidi chini na imepindia chini.

Shore-bluu
Blue Fly-catcher
Erannornis longicauda
Ni shore mrembo wa rangi ya kibuluu ambayo tumboni haikukolea. Mkia wake una ncha ndefu katikati.


Kielelezo Na. 175 Shomoro

Shorekishungi
Paradise Fly-catcher
Terpsiphone viridis
Shore wa kikahawia-chekundu mwenye mkia mrefu, kichwa cheusi chenye kishungi na duara jembamba jeupe kuzunguka jicho.

Shorewanda
Rufous Sparrow
Passer rufocinctus
Mnaana kahawia mwenye tako jekundu, milia meusi mgongoni na mraba mwekundu wa njano (chungwa) juu ya jicho.


Kielelezo Na. 176 Shorekishungi

Shorobo-bluu
Hartlaub’s Turaco
Turaco hartlaubi
Kama Shrobo-mwekundu lakini kishungi chake ni cha bluu.

Shorobo-mwekundu
Fischer’s Turaco
Turaco fischeri
Dura aliye kama Mwenge kwa kila hali, isipokuwa yeye ana kishungi chekundu na kifupi chenye ncha nyeupe.

Shundi
Black Coucal
Centropus toulou
Dudumizi mweusi wa mabwawa na kando ya mito.


Kielelezo Na. 177 Shorewanda

Silemaua
Lesser Jacana
Microparra capensis
Kung’wani mdogo wa kijivu ambaye hana kile kiraka samawati cha uso.


Kielelezo Na. 178 Shorobo-bluu

Sululu
Painted Snipe
Rostratula benghalensis
Ndege mdogo wa kando ya maji, jamii ya Kichonge, mwenye tumbo jeupe, shingo na koo la kahawia, mraba mpana mweusi kifuani, duara nyeupe iliyozungukajicho na kuelekea nyuma na domo refu lililopindia chini. Akiruka hakunji miguu.


Kielelezo Na. 179 Sululu

Taji
Crowned Crane
Balearica regulorum
Ndege wakubwa wa kijivu wenye miguu mirefu kama Korongo, ngozi nyeupe isiyo na manyoya chini yajicho na kisunzu kifupi na kipana kichwani.

Tai (Dekula)
Eagle
Falconidae
Ndege wakubwa wawindaji wenye makucha marefu na midomo mipana yenye ncha kali zilizopindia chini kama ndoana. (Tazama Pungu, Yowe).

Tambarazi
Spotted Creeper
Salpornis spilonota
Ndege mdogo wa kahawia, jamii ya Kigogota, mwenye madoa meupe mwili mzima na domo refu lililopinda kiasi.


Kielelezo Na. 180 Taji


Kielelezo Na. 181 Tambarazi

Tandawala
Bustard
Otididae
Ndege wakubwa kiasi wa kijivu, wa nyika, waliofanana na Korongo. Wana midomo midogo, kishungi kidogo na vidole vitatu.

Tandawala mdogo-mweupe
White- bellied Bustard
Eupo-dotis senegalensis
Tandawala mdogo wa kimanjano-kijivu mwenye tumbo jeupe na shingo samawati.

Tandawala mdogo-mweusi
Black-bellied Bustard
Lissortis melanogaster
Tandawala mdogo kahawia-kijivu mwenye tumbo jeusi. Jike lake limefanana na Tandawala-mdogo-mweupe lakini halina shingo samawati.

Tandawala-mkubwa
Greater (Kori) Bustard
Ardeotis kori
Huyu ni mkubwa kupita Karani na ana kisunzu na manyoya mengi meroro shingoni yanayoifanya shingo ionekane nene. Mkia wake ni mfupi. Juu ni kijivu, tumbo jeupe na mbawa zina mabaka meupe.


Kielelezo Na. 182 Tandawala mdogo-mweupe

Tapo
Cardinal Quelea
Quelea cardinalis
Yombiyombi mwenye kichwa chekundu sana, tumbo la rangi ya maziwa na domo la kijivu.

Tararita (Kidata)
Cut-throat
Amadina fasciata
Chiriku kahawia mwenye madoa na milia ya kijivu, tumbo jekundu na mraba mwekundu kama koo lililokatwa.

Teleka
Bulbul
Pynonotidae
Ndege kahawia, kijani-kijivu na njano; jamii ya Shore. (Pia tazama Kizelele).


Kielelezo Na. 183 Tandawala mdogo-mweusi

Tembere
Peregrine
Falco peregrinus
Tai mdogo wa kijivu-cheusi juu mwenye koo jeupe na tumbo la kijivu lenye madoa meusi.

Tetere
Dove
Columbidae
Njiwa wadogo. (Tazama Pugi)


Kielelezo na. 184 Tandawala-mkubwa

Timvi
African Barn-owl
Tylo alba
Bundi mdogo kahawia asiye na masikio, mwenye madoadoa, uso wenye sura ya moyo na tumbo jeupe. Ana kilio cha kutisha. (Tazama Babewana).

Tipitipi-kijani
Emerald Cuckoo
Chrysococcyx cupreus
Huyu ana tumbo la njano na mraba wa jicho.

Tipitipi-mweupe
Diric Cuckoo
Chrysococcyx caprius
Ni Mlemba wa kikahawia-kijani mwenye tumbo jeupe na mraba mweupe wa jicho.


Kielelezo Na. 185 Tapo

Tiva-mweupe
Tropical Boubou
Laniarius aethiopicus
Kipwe mdogo mweusi mwenye tumbo la maziwa na jicho la njano.


Kielelezo Na. 186 Tararita


Kielelezo Na. 187 Tembere

Tiva-mweusi
Slate-coloured Boubou
Laniarus funebris
Huyu ni mweusi.


Kielelezo Na. 188 Tiva-mweusi

Toboang’ombe (Mlakupe)-mwekundu
Red-billed Oxpecker
Buphagus erythorhynchus
Ndege mdogo kahawia mwenye domo jekundu na mviringo wa njano kuzunguka jicho ambaye hufuata na wanyama. Hula kupe.


Kielelezo Na. 189 Toboang’ombe-mwekundu

Toboang’ombe-njano
Yellow-billed Oxpecker
Buphagus africanus
Huyu ana domo la njano.


Kielelezo Na. 190 Toboang’ombe – njano

Tomboro
Harlequin Quail
Cotunix delegorguei
Ndege mdogo wa kikahawia-cheusi aliyefanana na Kwale, lakini mdogo zaidi, mwenye miraba miwili myeupe kooni (jike halina miraba) na milia myeupe.


Kielelezo Na. 191 Tomboro

Tongobofu
Bronze Mannikin
Spermestes cucullatus
Chiriku mdogo wa kijani-cheusi mwenye kichwa na mkia wa kijivu-cheusi, tumbo jeupe na tako jeupe lenye milia myeusi ya kukata. Huonekana kwa wingi kwenye ukoka wa milimani.


Kielelezo Na. 192 Tongobofu


Kielelezo Na. 193 Tumbusi

Tongokanga
Rufous Mannikm
Spermestes nigriceps
Jamii ya Tongobofu lakini mgongo wake mwekundu.

Tongosimba
Magpie Mannikin
Ameuresthes fringilloides
Jamii ya Tongobofu ambaye ana miraba myeupe na myeusi.

Totowo-mweupe
Black and White Cuckoo
Clamator jacobinus
Huyu ana tumbo jeupe na kisunzu. (Tazama Semkoko)

Totowo-mweusi
Black Cuckoo
Cuculus caffer
Mlemba mweusi wa vichaka vya mito na maziwa mwenye jicho la njano.

Tumbusi
Vulture
Aegypiidae
Ndege wakubwa wa kikahawia-kijivu wala mizoga wenye shingo na vichwa kipara na midomo mikubwa yenye ncha kali zilizopindia chini kama za Tai.

Tumbusi-mweupe
White-backed Vulture
Psendogypus africanus
Huyu ana kichwa na mdomo kijivu na takojeupe.

Tumbusi-njano
Egyptian Vulture
Neophron percnopterus
Huyu ni Tumbusi mdogo mweupe mwenye kichwa chenye manyoya na uso wa njano.

Tunguhina
Purple Grenadier
Granatma ianthinogaster
Jamii ya Tunguridi na Mshingi ambaye ni wa kahawia, ana tako samawati, mkia mweusi na domo jekundu.

Tunguridi
Cordon-bleu
Uraeginthus
Chiriku kahawia juu, chini na mkiani samawati, mwenye mraba mwekundu chini yajicho. Wa kusini mraba huu ni samawati.

Tutu
Pink-breasted Dove
Streptopelia lugeus
Tetere kijivu-cheusi, mwenye mraba mweusi begani na kiraka chekundu (kahawia) penye mbawa. (Tazama Pugi).


Kielelezo Na. 194 Tunguridi

Ukiki
Yellow-billed (green) Councal
Ceuthmochares aereus
Dudumizi kijani-kijivu wa msituni mwenye mraba samawati unaozunguka jicho na domo la njano. (Tazama Dudumizi)

Umbia
Golden Oriole
Oriolus auratus
Kama Kipwe lakini huyu ni njano kote, macho na mdomo mwekundu na ana msitari mweusi nyuma ya jicho. (Tazama Mramba).


Kielelezo Na. 195 Vuachwe-domohina

Undu
Ross’s Turaco
Musophaga rossae
Dura zambarau mwenye kisunzu chekundu, domo kubwa la njano, mraba mwekundu kwenve mbawa na kiraka cha njano jichoni. (Tazama Shorobo).

Upapasa
Dusky Night-jar
Caprimulgus fraenatus
Kipasuasanda mrembo mwenye mraba kahawia shingoni, madoadoa mengi meupe mbawani na mkia mweupe nchani. Aina yake ndiyo inayoonekana zaidi.


Kielelezo Na. 196 Yangevange

Vinago
Tambourine Dove
Tympanistria tympanistria
Tetere wa kikahawia-kijivu mwenye uso na tumbo jeupe na mraba mweupe penyejicho. (Tazama Pugi)

Vuachwe-domochini
Woodland King-fisher
Halcyon senegalensis
Kizamiadagaa mkubwa wa kibuluu mwenye domo jekundu juu na chinijeusi, na miguu ya machungwa.

Vuachwe-domohina
Mangrove King-fisher
Halcyon senegaloides
Huyu ana domo jekundu kote. Anapendelea vichaka vya pwani.

Vumatiti
Dwarf Bittern
Ardeirallus sturmii
Jamii ya Ngojamaliko lakini yeye ni kijivu-cheusi kote na shingo yake kijivu.

Yangeyange
Egret
Ardeidae (Egretta)
Kundi la ndege weupe wenye midomo ya njano wa jamii ya Kulasitara; Mfuatang’ombe ni mmoja wao.

Yange yange – domojeusi
Little Egret
Egretta garzetta
Huyu ana miguu myeusi, vidole vya njano na ni pekee mwenye domo jeusi.

Yangeyange -mdogo
Yellow-billed Egret
Mesophoyx intermedius
Huyu ana miguu myeusi kote.

Yangeyange-mkubwa
Great While Egret
Casmerodius albus
Kama Yangeyange-mdogo lakini ni mkubwa na ana kisunzu kirefu.

Wanda
Wood Dove
Turtur
Njiwa wadogo kahawia wa nyikani wenye mbawa madoa makubwa ya kijani na midomo myekundu. (Tazama Pugi).


Kielelezo Na. 197 Yowe

Wanda-njano
Blue-spotted Wood Dove
Turtur afer
Huyu ana domo la njano na miraba miwili myeusi mkiani.

Yakuti
Tacazze Sunbird
Nectarinia tacazze
Chozi mrembo kuliko wote wa kizambarau-chekundu kinachong’aa. Mkia wake una manyoya marefu ya kati kama wa mtilili.

Yombiyombi
Quelea
Quelea (Plocidae)
Jamii ya Pasuambegu ambao hutembea kwa wingi sana na kushambulia nafaka, hasa ulezi, mtama na uwele. Wana midomo mipana na mifupi. Tazama Tapo na Kivo. Huharibu tani nyingi za mazao kila mwaka na Umoja wa Mataifa una mpango maalum wa kuwasaka.


Kielelezo Na. 198 Zawaridi

Yowe (Kwazi)
Fish-Eagle
Cuncuma vocifer
Tai mkubwa mweusi mla samaki, pekee mwenye kichwa na mkia mweupe na tumbo la kikahawia- chekundu. Anapiga mayowe makubwa yanayosikika mbali.

Zawaridi
Melba-Finch (Pytilia)
Pytillia melba
Chiriku mdogo mrembo mwenye mbawa za kijani, kisogo kijivu, mdomo na mkia mwekundu, kifua cha njano na tumbo jeupe lenye milia ya mkato pembeni.


Kielelezo Na. 199 Zuakulu

Zuakulu
Black-collared Barbet
Lvbius torguatus
Kisigajiru mkubwa mwenye uso na koo jekundu, tumbo la njano, mraba mweusi kifuani ambao shingoni umepanuka na mbawa za kimanjano- kijivu. Mdomo wake unajino (sumeno) moja.

BOFYA HAPA KUONA PICHA>>>>>>>>>

error: Jisajili kupata uhuru zaidi !!