JIPIME KWA MASWALI YA USHAIRI

By , in MITIHANI I-IV MITIHANI V-VI on . Tagged width:
Swali la kwanza. 
Fafanua kwa hoja tatu kutoka kila diwani kati ya mbili ulizosoma ni kwa jinsi gani wasanii wa kazi hizo wamefanikiwa kuzungumzia suala la mapenzi katika jamii kwa namna tofauti.
Swali la pili.
Matumizi ya lugha ni nyenzo muhimu katika kufanikisha azma ya msanii kufikisha ujumbe kwa jamii. Thibitisha kauli hiyo kwa kutumia diwani mbili kati ya ulizosoma. Toa hoja tatu toka kila diwani.
Swali la tatu. 
Nafasi ya mwanamke ni jambo ambalo limekuwa likizungumziwa sana na wasanii wa kazi za fasihi. Toa hoja tatu kutoka kila diwani kuonesha jinsi wasanii wa kazi hizo walivyomtweza na kumkweza mwanamke kupitia kazi zao.
Swali la nne. 
Suala la ukombozi wa kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni ni miongoni mwa dhima za kifasihi ambazo waandishi wa diwani wameibua ndani ya kazi zao ili kujenga jamii mpya. Thibitisha dai hilo kwa kutoa hoja tatu kutoka kila diwani kati ya mbili ulizosoma.