JINSI YA KUTAMBUA MZIZI/KIINI KATIKA NENO

By , in Sarufi na Utumizi Wa Lugha on .

Mzizi au kiini cha neno huweza kubainika kwa kutumia mbinu zifuatazo:

  • Mbinu ya mnyambuliko/unyambulishaji

Neno husika hufanyiwa mnyambuliko kwa kubadili viambishi kadiri iwezekanavyo na kisha kuchunguza sehemu isiyobadilika katika maneno yaliyotokana na mnyambuliko (vinyambuo).

Mf:

Cheza ——- Mchezo

Mchezaji

Michezo                                   -chez-

Tumecheza

Walivyotuchezesha

 

  • Kuzingatia umoja na wingi

Mbinu hii hufaa zaidi kwa maneno ambayo ni nomino. Nomino zisizo na umoja na wingi aghalabu huwa ni maneno yaliyoundwa kwa mofimu moja hivyo si rahisi kupata mzizi na viambishi.

Mf:

Mtoto ——– watoto  (toto)

Mzee ——— wazee (zee)

Kifaranga —– vifaranga (faranga)

  • Kuzingatia muundo ndani wa neno

Vitenzi vingi vya Kiswahili huwa na muundo ndani na muundo nje. Ili kutambua mzizi wa kitenzi kwa urahisi ni vyema kukirudisha kitenzi katika muundo wake wa ndani. Kitenzi chenye asili ya kibantu muundo wake wa ndani huishia na irabu “a”. Kitenzi kikiwa katika muundo ndani na kuishia na irabu “a” basi hiyo irabu ikiondolewa kinachobakia huwa ndio mzizi.

Mfano:

Walipigana —————- piga ——– pig-

Tumemuimbia ———— imba ——- imb-

Wanasomeshwa ———- soma ——- som-

Iwapo kitenzi katika muundo wake wa ndani kitaishia na irabu tofauti na “a” basi yawezekana neno zima likawa mzizi au shina. Hali hiyo hutokea kwa vitenzi vyenye asili ya kigeni.

Mfano:

Waliosaliana ———- Sali

Walivyostarehe ——- starehe

Tulimuarifu ———— arif

Recommended articles