KISWAHILI 1 : JINSI YA KUJIBU MASWALI YA SEHEMU B : MATUMIZI YA SARUFI NA UTUMIZI WA LUGHA

By , in Kidato V-VI on . Tagged width:

JINSI YA KUJIBU MASWALI YA SEHEMU B : MATUMIZI YA SARUFI NA UTUMIZI WA LUGHA

 1. Kwa kutoa mifano, onesha maumbo mbalimbali ya kitenzi kishirikishi. (onesha

maumbo matano).

 

MAJIBU

(i) Kishirikishi –li-

Mfano:

 

 • Embe li bicho
 • Gari li bovu

(ii) Kishirikishi –u-

 • Wewe u mdogo
 • Baba u mkubwa

(iii) Umbo –i-

 • Mikono i mirefu
 • Shule i porini

 

(iv) Umbo –ki-

– Kisu ki kikali

– Kisahani ki kidogo

 

(v) Umbo –ndi- ambalo haliwezikusimama peke yake bali huambishwa kirejeshi kulingana na nomino husika.

– Tumaini ndiye mkubwa

– Watoto ndio wakorofi

– Ndizi ndizo mbivu

 

(vi) Umbo –ngali-

 • – Amani angali mtoto
 • – chakula kingali kibichi

(vii) Umbo -wa-

 • – Wazee wa wakali
 • – vijana wa wakorofi

 

(vii) Umbo –si- (huongezwa kiambishi rejeshi kulingana na nomino husika.

 • Yeye si mwanangu
 • Yeye ndiye mwanangu

 

(viii) Umbo –kuna-/ – hakuna-

 • Mbagala kuna mvua
 • Mbagala hakuna mvua

(viii) Umbo –yu-

 • Huyu yu mgonjwa
 • -Mzee yu hospitali

(ix) Umbo –ya-

 • – Maembe ya mabichi
 • – Mashati ya machafu
 1. (a) Eleza maana ya kishazi na utoe mifano.

MAJIBU

 • Kishazi ni tungo inayotawaliwa na kitenzi na yenye kutoa taarifa kamili au isiyo kamili. Kitenzi chenye kutoa taarifa kamili huzalisha kishazi huru na kile chenye taarifa isiyo kamili huzaaa kishazi tegemezi (K/Tg).

Mfano:

 • Baba analima (K/Hr)
 • Mtoto anayelia (K/Tg)

 

 • Fafanua sifa nne za kishazi tegemezi na utoe mifano kwa kila sifa.

 

Sifa za kishazi tegemezi

– Hakitoi taarifa kamili bila kuambatana na kishazi huru

Mfano:

 • Mtoto aliyeiba jana
 • Chumba kilichovunjwa

– Hutambulika kwa kuwa na viambishi rejeshi

Mfano:

 • Shule inayouzwa
 • Nyumbu aliyepigwa risasi

 

– Huweza kufutwa katika sentensi bila kuathiri maana

Mfano:

 • Mtoto anayelia amenyamaza
 • Mtoto amenyamaza

 

– Huweza kutokea kabla au baada ya kishazi huru

 • Mama aliondoka aliponiona
 • Mama aliponiona aliondoka

 

 1. Kwa kutoa mifano miwili kwa kila kazi bainisha kazi tano za “kwa” katika tungo za Kiswahili.

 

MAJIBU

 • Kuonesha mahali
 • Juma alienda kwa mwalimu
 • Sisi tutaenda kwa dada

 

 • Kuonesha namna au jinsi
 • Mgonjwa alikula kwa tabu
 • Vijana waliimba kwa madaha

 

 • Kuonesha uwiano
 • Walifunga magoli matatu kwa mawili
 • Watashindana wazee kwa vijana

 

 • Kuonesha sababu
 • Alifeli mtihani kwa uzembe
 • Utachelewa kwa uvivu

 

 • Kuonesha matumizi ya kitu
 • Tutaenda kwa basi
 • Utakula kwa kijiko

 

 • Kuonesha thamani
 • Alinunua kwa bei ghali
 • Atauza kwa gharama kubwa

 

 1. Nini maana ya mtindo wa lugha ya kiofisi/kikazi? Fafanua kwa mifano sifa nne (4) za mtindo wa lugha ya kiofisi/kikazi.

 

MAJIBU

 • Mtindo wa lugha ya kiofisi/kikazi ni mtindo unaotumika katika mawasiliano rasmi ambayo hupatikana katika ofisi au mahali popote pa kazi, mikataba, matini za kisheria, matangazo ya vikao, ripoti za mikutano, mahakamani, n.k.

 

 • Sifa za mindo wa lugha ya kiofisi/kikazi ni kama vile:

 

 • Usahihi wa mambo yanayojadiliwa (ushahidi)
 • Matumizi ya istilahi maalumu zinazohusu mambo ya kiofisi
 • Hakuna matumizi ya misimu, mafumbo, tafsida (hutumia lugha sanifu)
 • Matumizi ya vifupisho hasa majina ya mashirika ya kimataifa kama vile UNO, ILO, UNICEF, IMF, UNESCO, n.k (Majina ya watu hayaruhusiwi kufupishwa)