JE, KISWAHILI HAKINA MSAMIATI WA KUTOSHA?

By , in Kiswahili cha Kompyuta on .

Najua sisi sote humu ndani ya hili kundi sogozi tunamiliki simu tamba. Tuweni makini kwani kutumia sikanu zetu mkondoni kunaweza wapa mwanya wezi wa mtandaoni kutuibia. Wezi hutuma maunzi laini yanayoweza kuharibu kitumi chako au kuingilia makavazi ya sikanu yako. Wakishatuma maunzi laini hayo nawe pasi na kujua ukibofya kiungo kilichobeba maunzi laini unakuwa umeshapakua na kusanidi mtaliga wenye uwezo wa kubadili au kughushi neno siri lako na hivyo kunyima uwezo wa kuitumia sikanu yako kwa kuifanya puku kushindwa kutambua amri unazoipatia baobonye ya kiwambagusa cha sikanu yako.

⬇⬇⬇⬇⬇⬇⬇⬇⬇⬇⬇⬇
Tafsiri ya maneno hayo

1. Kundi sogozi = chatting group
2. Sikanu = smartphone
3. Kitumi=device
4. Maunzi laini=software
5. Kiungo=link
6. Kusanidi=install
7. Mtaliga=virus
8. Neno Siri=keyword
9. Puku=mouse
10.Baobonye=keyboard
11. Kiwamba gusa=touch screen
12. Makavazi=archives
13. Simu tamba=mobile phone
14. Mkondoni=online
15. Pakua=download

Recommended articles