DHIMA YA UHURU WA MWANDISHI

By , in Kidato V-VI on .

  • Mwandishi atakuwa huru kuikosoa jamii au tabaka lolote litakaloenda kinyume nautaratibu wa jamii bila matatizo.Mwandishi atakuwa huru kuonyesha dhuluma, ukatili na ujangili unaofanywa katika jamii na tabaka lolote bila matatizo yoyote.
  • Kukiwa na uhuru wa mwandishi, msanii atakuwa na falsafa inayoeleweka pamoja na utashiwake.Hii itamfanya mwandishi awe na msimamo unaoeleweka.Msimamo  wake utamsaidia kuifundisha na kuielimisha jamii bila uoga.Ataijiulisha jamii hali yake na ataonesha jamii njia za kufikia haja na kutatua matatizo ya jamii bila uoga
  • Mwandishi atakuwa huru kutoa mwongozo katika jamii kwa kuikomboa jamii kutoka katika fikra mbovu za kugandamizwa,kunyonywa na kuonewa na tabaka tawala ili jamii ipate haki na heshima bila woga wa kuliondoa tabaka ambalo ndilo lenye mamlaka yote katika jamii.
  • Uandishi wa kikasuku utapungua, waandishi au wasanii huacha tabia ya kuwa vipaza sauti vya tabaka fulani katika jamii, wasanii makasuku huandika mambo bila kufikiri na kurudiarudia  mawazo yaliyokwisha semwa na wanasiasa majukwaani bila fikra mpya kwa hali hii hupotosha jamii.Hivyo kunapokuwa na uhuru wa mwandishi wa kutosha hali hii haiwezi kutokea kwa sababu mwandishi ataandika mambo mbalimbali yanayojitokeza katika jamii na hataweza kujikomba au kujipendekeza kwa tabaka tawala lenye mamlaka yote katika jamii.
  • Kunapokuwa na uhuru wa mwandishi fasihi inakuwa chombo cha kuikomboa jamii kiuchumi,kisiasa, kiutamaduni na kifikra (kimawazo). katika jamii ya kitabaka fasihi ni mali ya tabaka tawala na hutumia fasihi kutetea na kulinda maslahi yao.Hivyo inapokuwa mali ya jamii nzima inatumiwa na jamii hiyo katika kuwakomboa wanajamii wote.
  • Kunapokuwa na uhuru wa mwandishi, mwandishi anakuwa huru kuichokoza na kuisukasuka (kuichochea)jamii bila matatizo yeyote. Mwandishi atachokoza jamii ya wakulima na wafanyakazi kufikiri ili waweze kulichunguza tabaka tawala kwa jicho pevu na kutoa hadharani uozo uliopo katika kunyonywa, kupuuzwa,kuonewa, kugandamizwa na kunyanyaswa na tabaka tawala
  • Mwandishi atakuwa huru kuelimisha na kuishauri jamii katika mambo muhimu yanayojitokeza katika jamii bila woga.Mwandishi ataishauri jamii kuhusiana na mambo kama vile afya, elimu na ichague mambo gani yanafaa kuhifadhiwa na yapi hayafai vile vile msanii anakuwa huru kuirekebisha jamii bila woga kwa kuangalia yapi ni mazuri na yapi ni mabovu yanayotendeka katika jamii
Recommended articles