DHIMA YA MHAKIKI WA FASIHI

By , in Kidato V-VI on .
  1. Kuchambua na kuweka wazi funzo litolewalo na kazi ya fasihi.
  2. Kuchambua na kufafanua taswira (picha za kisanii) zilizotumika katika kazi ya mwandishi.
  1. Kumshauri na kumtia moyo mwandishi ili afanye kazi bora zaidi (hivyo mhakiki pia ni mwalimu wa mwandishi)
  2. Kumwelekeza na kumchochea msomaji kusoma na kupata faida zaidi ya ambayo angeipata pasipo dira ya mhakiki (mhakiki ni mwalimu na daraja kati ya mwandishi na jamii)
  1. Kuhimiza na kushirikisha fikra za kihakiki katika kazi za fasihi.
  1. Kukuza kiwango cha utunzi na usomaji wa kazi za fasihi.
  1. Kutafuta na kuweka sawa nadharia za fasihi teule.
  1. Kuthamini na kuheshimu kazi za waandishi kwa kuzitendea haki
Recommended articles