DHANA NA DHIMA YA -O- REJESHI

By , in Kidato I-IV Kidato V-VI on .

Fasili: -0-rejeshi ni kiambishi cha mtenda au mtendwa ambacho hujitokeza katika kitenzi au amba- ili kuonesha dhana ya urejeshi. Urejeshi huo hufuata  mfumo wa upatanishi wa kisarufi  yaani mfumo wa ngeli. Ngeli ni utaratibu wa kupanga majina ya Kiwahili katika makundi yanayofanana. Kiambishi hiki  hujiegemeza  kwenye kiambishi ngeli cha nomino iliyotajwa.

Viambishi vya –o- rejeshi ni kama vile -ye-, -o-,

-cho, -mo-, -vyo-

Kwa mfano:

  1. Mtu  a-li-ye-iba
  2. Watu wa-li-o-iba

Katika mifani (i) na (ii)  -ye- na -o- ndivyo vinavyoitwa viambishi vya -o- rejeshi.

Katika -o- rejeshi vitenzi hubeba viambishi ngeli vyenye kiangami -o- isipokuwa kama nomino iliyotajwa  ni ngeli ya kwanza umoja. Urejeshi wa ngeli hiyo hutumia -e- badala ya

-o-. Hivyo, -ye- ni -o- rejeshi kwa kwa inaangukia kwenye ngeli ya kwanza (YU/A-WA) hata kama haina -O-

Swali: Taja mazingira matatu ya kisarufi ya utokeaji wa -o- rejeshi katika tungo. Kiambishi cha -o- rejeshi hujitokeza katika mazingira yafuatayo:

Mosi hujitokeza  kabla ya mzizi wa kitenzi.

Kwa mfano:

  1. Mzizi wa kitenzi ni -li-; kiambishi -ye-kimejitokeza  kabla ya mzizi wa kitenzi na ndivyo ilivyo katika mfano wa ii ambapo mzizi wa kitenzi ni -imb-, hivyo kiambishi rejeshi –vyo-  kimejitokeza kabla ya mzizi huo.
  2. Pili, -o- rejeshi hutokea  baada ya mzizi wa kitenzi. Mfano (ii) -j- ndiyo mzizi wa kitenzi, kirejeshi –o- kimejitokeza baada ya mzizi wa kitenzi.
  3. Mwisho –o- rejeshi hujitokeza katika shina amba-. Shina hili huongezewa viambihi vya -o- rejeshi na kupata neno lionyeshalo urejeshi. Hapa tunapata maneno kama ambalo, ambaye, ambacho, nk. haya ndiyo mazingira ya utokeaji wa -o- rejeshi. Zifuatzo ni dhima tano za -o- rejeshi:
  4. Huunganisha tungo mbili zenye dhana moja. Mfano:(a) Mwalimu amefundisha. (b) Mwalimu amehama.

Kutokana na tungo hizi mbili tunaweza kupata  tungo moja: Mwalimu anayefundisha amehama.

  1. Huonyesha namna tendo linavyotendeka.

Mfano: Anavyokula ananitamanisha.

  1. Kuonyesha mahali ambapo tendo hutendeka. Mfano: “Anamolala” (ndani).
  2. Hudokesha nafsi ya mtenda au mtendwa wa jambo. Mfano: Walioiba (nafsi ya III wingi).
  3. Hudokeza idadi (umoja na wingi). Mfano: Anayecheka (umoja), wanaocheka (wingi).
Facebook Comments
Donate
Recommended articles