CHANGAMOTO YA TAFSIRI KATIKA SIMU ZA RUNUNU

By , in TAFSIRI/UKALIMANI on .

CHANGAMOTO YA TAFSIRI KATIKA SIMU ZA RUNUNU

Simu za rununu hutekeleza jukumu kubwa la mawasiliano.Hali hii hurahisisha mitagusano baina ya watu. Mawasiliano haya hupitia maongezi,jumbe fupi,twita na mitandao mingine.Simu hizi vile vile husaidia katika uhawilishi na usambazi wa pesa.Mashirika yanayomiliki simu hizi yanafanya juhudi kubwa za kuendeleza Kiswahili kwa kuitumia katika kueleza huduma muhimu wanazotoa kama vile:mpesa,pesa mkononi,M-kopa n.k. Ni jambo la kuvunja moyo kuona mashirika haya yakitumia tafsiri isiyofaa. Tafsiri huwa ni muhimu kwa kuwa husaidia watu wasioelewa lugha asili kupokea ujumbe katika lugha pokezi. Ni muhimu hata hivyo kuzingatia tafsiri faafu ili kuufikisha uju namna ilivyokusudiwa.Tafsiri inapokuwa mbovu inaweza kupotosha ujumbe.Aidha, inaweza kuendeleza lugha isiyo sanifu na hata kuathiri wanafunzi katika masomo yao na matokeo ya mitihani.Makala haya yanajadili changamoto zinazojitokeza katika hizi. Inajadili tafsiri ambazo ni mbovu na kupendekeza tafsiri faafu inapowezekana.Tunatoa mifano kutoka mashirika ya Safaricom, Airtel na Orange, Tigo, Vodacom, n.k.Tumeteua mashirika haya kutokana na idadi kubwa ya watumizi.Tunaangalia huduma tofauti zinazotolewa na mashirika haya ambazo zimetafsiriwa.Makala haya yanapendekeza njia tofauti za kupunguza hali hii.Tuna imani kuwa mapendekezo haya yataweza kuwasaidia watawala wa mashirika kulipa suala la tafsiri uzito unaostahiki.Tafsiri itaendelezwa na watu ambao wana ujuzi wa taaluma ila si yeyote anayedhaniwa kuwa anaweza kuzungumza Kiswahili.

Recommended articles
error: Jisajili kupata uhuru zaidi !!