CHALUFAKITA WAITUNUKU REDIO TEHRAN TUNZO YA KUTUNZA LUGHA YA KISWAHILI

By , in Zote on . Tagged width:

SAUTI, Idhaa ya Kiswahili Redio Tehran yatunukiwa tuzo ya kulinda lugha ya Kiswahili na chama cha Lugha na Fasihi Tanzania

Chama cha Lugha na Fasihi ya Kiswahili nchini Tanzania CHALUFAKITA kimeitunuku Idhaa ya Kiswahili Sauti ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran zawadi maalumu ya shahada ya kutunza lugha ya Kiswahili.
Hatua hiyo imekuja kutokana na mchango mkubwa wa Redio Tehran katika kuenzi na kutumia fasihi ya lugha hiyo katika matangazo yake.

Cheti kilichotolewa kwa ajili ya Redio Tehran

Zawadi hiyo imetolewa katika kongamano la siku tatu la Kiswahili lililofanyika visiwani Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi wa serikali, waandishi na wataalamu wa Kiswahili kutoka Afrika Mashariki. CHANZO >>>>>>>