ASILI YA SANAA: Sehemu ya pili

By , in Fasihi Simulizi on . Tagged width: ,

ASILI YA SANAA: Sehemu ya pili

S.J. Ntiro

Sanaa ni matokeo ya dhana ya mawazo ya msanil ili sanaa lundwe msanil ni lazima awe na dhana kamili kichwani mwake kuhusu sanaa anazokusudla kuunda. Baadhl yasanaazenyemaana ni zileambazo mtazamajl aklzlona anazlelewa mara moja maana yake bila ya kuuliza msanil aeleze alichokusudia alipozitengeneza. Kuna sanaa za alna nylngl. Sanaa zilizo maarufu ni za rangl, za magogo ya mitl, za mawe na za udongo wa mflnyanzi kwa kutaja mlfano mlchache tu.

Sanaaza rangl zlnaweza kuwa nawatu, wanyama wa porini na wa nyumbanl, mlti mikubwa na misitu, nyanda zenye nyasl, milima, majl ya baharl na ya mazlwa makubwa, mazinglra ya mvua na ya ukame, hali ya watu wenye haslra na wenye furaha, desturl na tabia za watu zilizochongwa kwenye magogo ya miti au zilizoundwa katika udongo wa mflnyanzi zinaweza kuwa za watu, wanyama wa mlfugo ya nyumbani au porini au vltu vlsivyo na uhai vya matumizi ya nyumbani kama vitl vya kukalia, flmbo za kutembelea, vitanda vya kulalia, milango ya nyumba, vyungu vya kupikia chakula au kuwekea maji na pombe. Ili sanaa hizi zitokee msanil anahitaji vifaa vya kutumia kama magogo ya miti, mawe au udongo wa mfinyanzl, tezo, patasi, msumeno, nyundo za mlti na za chuma, na vinginevyo.

Msanil lazima awe na ujuzi kamili wa kutumia vyombo hlvi. Akiwa ni mchoraji inambidi atayarishe mahali pa kuchorea sanaa. Kama ni mchongajl ni lazima achague lile gogo ambalo litatosha sanaa yake. Mchongajl anajua kwamba aklchonga sehemu fulani hawezi kuirudishia. Lakini akitumia udongo wa mfinyanzi anaweza kuanza kuumba sanaa yake hatua kwa hatua, akiongeza sehemu zake ndogo ndogo. Hapo akikosea sehemu fulani anaweza kuiondoa na kuirudlshla.

Msanii anajua sanaa zenye manufaa ni zile zilizo na maana katika malsha yake na yale ya wenzake. Ni sanaa zinazoeleza shughuli, mawazo na busara za watu. Ni sanaa zenye hadhi ya tabia za watu ndizo zinazompasa msanli azlfurahle na kujlvunia.

Haiwezekani kabisa msanii kuunda – sanaa zinazoonyesha hali ya maisha ya watu bila kufshi nao. Ni muhimukabisa msanii awe ameelewa matatizo na furaha za maisha ya watu kwa kulshi nao wala sl kusoma vitabu au kusomeshwa shuleni juu ya maisha yawatu hao.

Hata kama msanii ameishi maisha hayo na watu kama ameyadharau kwa njia yoyote hawezi kutengeneza sanaa zinazostahili sifa za watu hao. Msanii halisi ni lazima ajivunie maisha na desturi za watu ndlpo atakapoweza kutengeneza sanaa zitakazofaulu kuonyesha desturi zao bila kukosea.

Sanaa za msanii mashuhuri zinawatia moyo wasanii wenzake kwa kuwatia moyo hatusemi kwamba wanamwiga moja kwa moja ila wanajiuliza’maswali kwamba ikiwa mwenzao ameweza kutengeneza sanaa zinazowashangaza watu wakizitazama kwa nini wao wasiweze kufaulu kama yeye? Kutokana na kujiuliza hivyo watafanya bidii na bila shaka watafanikiwa.

Msanii halisi ana uwezo wa aina mbili, ule wa kuzaliwa na wa pili wa bidii zake. Bila shaka kipaji cha kuzaliwa ni cha maana sana katika maisha ya msanii, lakini bila bidii kipaji hicho hakimfikishi mahali popote. Kipaji cha msanii ni lazima kiende pamoja na ari, bldii na kutoridhika hatua hadi hatua mpaka amefikia ngazi ya juu sana ya maendeleo yake ya usanii.

Tunapotazama historia ya wasanii tunaona kwamba wasanii wameishi pamoja, wakishirikiana kimawazo na kupeana moyo wakati wote wa shughuli zao. Lugha yao ni ya kisanii. Mawazo yao ni ya kuelewana kisanii, kwa hiyo popote walipo wanaishi maishayafurahapamoja.

Ni kweli kabisa kusema ujuzi wa sanaa unaweza kurithiwa na mtoto kutoka kwa baba yake mzazi. Lakini sl kweli kusema kwamba watoto wote wa baba huyo ambaye alikuwa msanii maarufu watakuwa wasanil. Wakati mwlngine hutokea asizae hata mtoto mmoja msanii kama yeye n’a wakati mwingine hutokea miongoni mwa watoto wake sita au saba akatokea mtoto mmoja tu akawa msanii kama baba yake.

Wakati mwingine hutokea sehemu fulani ya nchi, kwa sababu zisizoeleweka, ikawa na wasanii wengi kuliko sehemu zingine za nchi. Na wakati mwingine katika historia ya nchi kabila fulani linaweza kuwa na wasanii wengi maarufu kuliko makabila mengine katika nchi ile ile. Haya ni mambo ambayo sisi binadamu tunaweza kueleza. Na kwa upande wetu tunafurahi tunapopewa baraka ya kuwa na wasanii maarufu katika nchi yetu.

Maanaya Sanaa katika Malsha ya Mtanzania

Sanaa ina maana kubwa na pana katika maisha ya Mtanzania. Sanaa ni kitambulisho cha Mtanzania mahali popote duniani. Sanaa nzuri, iliyo na hadhi ya kusudi la msanii ni ya pekee na haiwezi kuwako nyingine kama hiyo. Sanaa ya namna hiyo ni ya maana kwa msanii na kwa Watanzania wenzake.

Mtanzania akizitembelea nchi za nje na kwa bahati nzuri akiiona sanaa ya Tanzania katika maonyesho ya sanaa za nchi nyingine ataltambua mara moja bila kuambiwa na mtu. Ataanza kulelezea sanaa hlyo na wageni watamsikiliza maelezo yake kwa kuwa ni urlthl wa nchi yake.

Ukitembelea nchini Tanzania na kukutana na wafinyanzi wa vyungu watakushangaza waklkuelezea jinsl wanavyoheshimu mahali wanapochlmba udongo wao. Wafinyanzi hao ambao wanatoka katika kijiji chao, msituni au mlimani au kwenye mtelemko wa maji. Kwa ajili ya kuchimba udongo hapo, vlzazl hata vizazi, shimo huwa kubwa na pana. Waflnyanzl kutoka kijiji kingine, hata wasipoambiwa kwambamahali hapa ni pa wafinyanzl wengine waklpatazama tu watajua pana wenyewe, na hawatapagusa. Hakuna ruhusa mgeni yeyote kutoka Tanzania au nje ya Tanzania kuonyeshwa mahali hapa kwa kuwa udongo unaochimbwa hapa unatumiwa na wafinyanzl wa pale tu kwa kuumbia vitu vyao. Kule Narumu, Kilimanjaro, kuna mahali pa aina hii. Mahali pengine ni Pare ya Kusini. Kwa hiyo ni mahali pa heshima na udongo unaochimbwa pale lazima uwe wa manufaa kwa kuumbiavitu vyenye utashi wa waflnyanzl nawajamii kwaujumla.

Msanii akisha iunda sanaa yake na Ikiwa nzurl, sanaa ya uchoraji, uchongajl au ya udongo wa mfinyanzi, basi wananchi wanaipokea na kujivuniakwa kuwa imetengenezwa na msanii wao. Ni heshima kubwa kwa msanii ikiwa sanaa yake inapokelewa namnahii.

Msingi wa Sanaa Tanzania

Sanaa katika Tanzania zina msingi wa miaka mingi kuliko jambo lingine lolote. Tangu miaka iliyopita babu zetu walikuwa wakitumia sanaa za aina zote kwa kuonyes ha vitendo vya wakati wao.

Wasanii wa wakati huo walituachia maelezo kamili ambayo tunayatumia kujifunza historia ya kaleyababu zetu. Kama wasanii hawa wasingefanya hlvyo leo tusingeweza kujifunza sehemu mojawapo ya historia ya Tanzania. Kwa hiyo inatubidi tuheshimu kazi za wasanii wetu wa kale na kutoa shukrani nyingl kwamba hata enzl hizo zilikuwa na wasanii. Kutokana na elimu hiyo ya wasanii wa kale ni lazima tuelewe kwamba wasanii wa Tanzania ya leo wanajenga msingl wa historiayawatu waTanzaniaya baadaye.

Katika Wilaya ya Kondoa tuna picha za mapangoni zilizochorwa na wasanii wa Tanzania. Sanaa zenye watu na wanyama wa porini zilichorwa miaka mia tano iliyopita. Picha hizi, ambazo tunaweza kuziona leo, zilichorwausoni mwa majabali ya mapango, babu zetu walipokuwawakiishi.


1. Picha ya mtoto wa kike anayechukuliwa ili aolewe.

Kuna sanaa zinazoonyesha maisha ya watu wa wakati huo. Sanaa hiyo hapo juu ina watu watano mwanamke katikati wanaume wawili waliojifunika nyuso upande wa kulia na wanaume wengine wawili wasiojifunika nyuso upande wa kushoto. Wanaume wa upande wa kulia wanamvuta mwanamke ili wampeleke kwao aolewe. Wale wanaume wawili wa upande mwingine wanamzuia mwanamke ambaye ni’ mwanawao asiolewe. Hii sanaa inatufundisha mila za babu zetu za wakati huo. Baada ya wazazi wa pande zote mbili kukubaliana mtoto aolewe na mtoto mwenyewe akikubali kuolewa, siku ya mtoto huyo kuchukuliwa ni lazima nguvu itumike na wale wa nyumbani kwake wamzuie kwa kuonyesha walimpenda mwanawao. Mila hii bado tunayo kila mahali Tanzania.


2. Kongoni aliyepigwa mshale na mwindaji

Katika picha Na. 2 tunamwona Kongoni akiwa na mshale wa mwindaji mwilini mwake. Damu inatiririka kutokamwilini na huku anaumiasana. Kwaupande wa kulia anaonekana mwindajl baada ya kutupa mshale akiwa na upinde mkononi. Picha hii inadhihirisha kwamba sanaa ilikuwa na nafasi kubwa katika maisha yakilasiku tangu enzi za maisha ya mapangoni. Picha Na. 3 nayo ilichorwa kwa madhymuni hayohayo.


3. Faru aliyechorwa kwa kalamu

Wataalamu wa historla ya kale kwa kutumia sanaa hizi wameweza kutupa miaka ya binadamu walivyolshi. Kazi iliyobaki sasa ni kutumia masalia ya vitu vilivyotumiwa kama mifupa, vyungu, ili kuonyesha shughuli nyingine za maisha ya watu wa wakati huo.

Wakati fulani, ambao haujajulikana vizuri, babu zetu walianza kuoridoka mapangom na kuishi porini, wakaanza kujenga nyumba za kuishi kama tujuavyo leo. Wakati huo waliendelea ‘na sanaa zao kwa kupamba kuta na milango ya nyumba zao, viti vya kukalia, ngao, mitungi ya kuwekea maji na pombe.

Kuanzia sanaa za mapangoni za Wilayaya Kondoa na uendelezaji wa vitu vlngl wakati watu walipoishi maisha ya kawaida mpaka leo, ndiyo msingi wa sanaa zetu Tanzania. Msingi huo uko katika milanadesturi za watuwaTanzania.

Matumizi ya Sanaa katika Maisha ya Mtanzania

Katika historia ya watu wa Tanzania hakuna sanaa zilizotengenezwa bila sababu maalum katika maisha ya watu. Tanzania kote bila shaka zamani alikuwako mchoraji aliyetimiza mahitaji ya wanakijiji. Mwanakijiji humwona mganga na kumwarifu kwamba shida itakwisha ikiwa atatengenezewa sanamu ya babu yake ambaye atamshughulikia ili matatizo yake ya maradhi yaishe. Basi mwanakijiji huenda kwa mchongaji na kumwelezea matatizo yake na kumwarifu jinsi alivyotumwa na mganga. Mwanakijiji akiisha mweleza mchongaji humchongea sanamu ambayo inafafana na babu yake kutokana na maelezo aliyopewa. Akimaliza kumchongea humkabidhi mwanakijiji sanamu yababu yake. Sanamu ya babu huyo huchukuliwa na mganga nakuwekwa mahali patambiko.

Usiku wa manane yule mganga akisimama mbele ya tambiko, na mwanakijiji akisimama ubavuni mwake kimya, humwita babu yake mwanakijiji na kumwomba aonane na mwanae ili amwombe amsamehe makosa yake ili (yeye au mkewe au mwanawe) mgonjwa apone. Wakati huo huo mganga humkabidhi sehemu fulani za nyama ya kondoo mweusi au mweupe na kuziweka kwenye tambiko mbele yake. Mwishowe wote wawili wanaondoka. Kwa kweli visehemu vya nyama huliwa na wanyamawaporini lakini huaminika kwambayulebabu ndiye aliyevila vile visehemu vya nyama, kwa hiyo alimkubalia mwanaye maombi yake. Huu ni mfano wa kuonyesha jinsi sanaa inavyotumiwa katika maisha ya Mtanzania.

Wamakonde ambao ni wachongaji mashuhuri Tanzania walichongamichongp ya miti yakufunikauso wa mtu ambao ulitiwa umaridadi mzuri ya kupendekeza tangu miaka iliyopita katika historia ndefu ya kabila lao. Uchongaji wa mchongo huu ulifuata umbile la mchezaji kiongozi wa hadithi ya kijadi. Kiongozi huyu ndiye aliyejua kucheza akifuata muziki wa hadithi hiyo. Wachezaji wengine wote walimfuata huyo mchezaji kiongozi. Pia muziki uliopigwa ulikuwa na kikundi kingine pembeni, wakati wapiga muziki waljpokuwa wakifuata muziki wa hadithi. Sanamu ya kuvaa usoni ilichongwa kwa sababu ya michezo, ambayo ilikuwa na sababu kamili. Kama ilivyo katika nchi zote za AfrikaSanamu yausoni (lipiku) Sanaayamsingi, na siku zote ilichongwa ili itumike, siyo itazamwe na kupendezawatazamaj! machoni.

Wasukuma hutumia sanaa za uchoraji kwa madhumuni tofauti kabisakwa kulinganishanayaleya Wamakonde. Wasukuma wana chama chao cha wachezaji wa nyoka. Msukuma akitaka kuwa mwanachama lazima alipe ada kwanza ndipo aingie katika masomo baada ya kula kiapo kwamba atakuwa mwanachama mwaminifu ambaye atafuata mafunzo kwa dhati na kwamba hatatoa siri za chama kwa mtu yeyotenjeyaChamanakwambaakitoasiri njeatakufa. Mafunzo huchukua muda mfupi au mrefu ukitegemea ari na bidii ya mwanachama. Mwanachama mpya anajulishwa kwamba chama kina mafunzo ya aina mbalimbali; ukamataji wa nyoka, matibabu ya watu walioumwa na nyoka, uchoraji wa sanaa kwenye kuta za nyumba za kufundishia na kadhalika. Nyumba za kufundishia zinaweza kuwa vibanda vilivyojengwa na kubomolewa baada ya muda wa mafunzo, au nyumba fulani katika kijiji zilizochaguliwa na chama. Jambo la msingi kuhusu muda wa mafunzo ni kufundisha hadithi. Hadithi ikiisha eleweka mwalimu wa sanaa anafundisha wanachama wapya namna ya kuchagua picha ambazo watachora ili zieleze hadithi waliyojifunza. Picha hizo zitakazochaguliwa zitakuwa zile ambazo zltawezekana kuchorwa na mtazamaji aklzitazama aelewe hadithi yake. Plcha zlkisha eleweka wachoraji huenda porini na kutafuta rangl mbalimbali, nyinglne za maganda ya mltl, majani ya mitl, mbegu na mlzlzl ya mltl. Pla walitafuta gundi ya namna ya utomvu, kutoka miti fulani ambayo wailitumia kwa kushikia rangl kwenye uso wa ukuta. Baada ya mwalimu wa sanaa kumaliza uchoraji wa sanaa za ukutani humkabidhi mwalimu wa mafunzo plcha hizo zaukutani. Mwalimu wa mafunzo hutumia sanaa hizi za ukutani kwa kuwafundisha wanafunzi wake mpaka wamezlelewa, kila moja, na jinsl zilivyotumiwa katika hadlthl na mwalimu wa sanaa na wanafunzl wake. Ili shughuli za uchoraji ziende sawasawa kama zilivyopangwa ni lazima mwalimu wa uchoraji ashirlklane vizuri na mwalimu wa mafunzo. Wakati mwlnglne husaidiana na msaada huu hutiliwa moyo katika mpango mzima wa chama cha wachezaji wa nyoka.

Mafunzo ya elimu ya Sanaa yatolewe pamoja na elimu kwa ujumla katika ngazi mbalimbali za elimu. Hapo hapo ndipo utaratibu wa mafunzo utatengenezwa. Wachongaji watafundishwa kuchonga vitu kutokana na historia, hadithi na mazingira ya nyumbani kwao. Watafundishwa namna nzuri ya kuchagua magogo yatakayofaa kwa michongo yao na vyombo vya asili. Mafunzo kuhusu uchoraji na uumbaji yatazlngatlwa namna hiyo hiyo.


4. Ilandula Igulu.

Shetani wa alfajiri. Mkongojo alioshika unawaka moto na ni alama ya kupata kwa jua. Ana paka wa porini ambaye anamfuata popote aendapo. Picha hii imechorwa na Msukuma kwenye ukuta wa nyumba za mafunzo ya wachezaji wa nyoka.

Ni rahisi kuficha mipango ya chama ya mafunzo ya uchoraji lakini ni vigumu zaidi kuficha mafunzo ya waimbaji na wachezaji. Waimbaji na wachezaji wanapofanya mazoezi yao katika vibanda vyao ni lazima sauti zao zisikike nje ya vibanda hivyo. Hata hivyo wanachama wote hujaribu kwa bldii zao zote kuweka mipango yao yote katika hali ya siri kutoka mwanzo hadi mwisho. Matumizi ya sanaa katika ·michezo ya wanachama wa chama cha wachezaji wa nvoka ni ya juu sana


5. Yahitinde

Yahitinde (Picha Na. 5) ni mchezajl wa nyoka aliyeishi miaka mingi iliyopita. Alijulikana sana kwa mafunzo yake aliyotoakwawanafunzi wapyawachama cha wachezaji wa nyoka. Mafunzo ya mwalimu huyu Msukuma yalihusika na ukamataji wa nyoka.

Uthamlni wa sanaa katika Tanzania ni wa namna mbalimbali kwa kutegemea ni watu gani wanaohusika na mahali walipo.

Watu ambao hawakufundlshwa utaalemu wa uthamini wa sanaa wanaliona jambo hili ni kama miujiza. Hawawezi kuamini kwamba binadamu mwenzake huchora, kuchonga au huumba sanaa ya mtu au mnyama. Kama utaalamu wa namna hiyo upo basl ni wa mtaalamu wa juu ya wataalamu wa kawaida.

Kama watu wanaohusika na uthamini wanaishi sehemu za mwambao, kwa desturi hutilia mkazo uthamini wavitu kamamiti navitu vinginevyo.

Ikiwa watu wanaohusika ni wale waliopata mafunzo ya juu katika somo hili, basi kazi hii huwa rahisi na ya kufurahisha. Kwanza wanaitazama sanaa inayohusika kutokana na msanii aliyeichora sanaa hiyo. Pili wanatazama uhusiano wasanaa hiyo najamii wa msanii. Halafu wanatazama utaalamu wake katika kuchora sanaa hiyo. Kama ni sanaa ya uchoraji wa rangi wanaangalia Jinsi alivyotumia rangi hizo. Kama ni sanaa ya kuchonga mchongaji ametumia gogo lililotosha urefu na upana wa sanaa aliyokusudia kuchonga.

Kwa ujumla sanaa nzuri ya aina yoyote Tanzania hupewa sifa inayostahili. Watu wanaona ujuzi wa sanaani wapekee.Siku hizi kwaajili yamwamko mzuri wa siasa yetu ya “Ujamaa na Kujitegemea” ambayo imeenea nchini kote watu wanaona kazi ya wasanii kuwa ni mfano mzuri wa siasa hii. Pia wanao wasanii na wataalamu ambao wanatangaza sifa nzuri ya nchi yetu. Watalii na wageni kutoka nchi za nje huvutiwa na sanaa nzuri za Tanzania kwa kuwa ndizo zinazoonyesha jinsi watu wa Tanzania wanavyoishi na kuongoza mambo ya nchi yao wenyewe. Sanaa hizi nzuri zinaonyesha shughuli za Watanzania vizuri zaidi kuliko maandishi ya vitabu na kuliko hotuba hata zikiwa nzuri namna gani, kama picha Na. 6 inavyoonyesha. Sababu yake hapa ni kwa kuwa badala ya kutumia lugha ya maneno msanii anatumia jinsi mtazamaji anavyotumia macho ya rohoni mwake na kuona kile kitu ambacho fikra zake zimeona. Tunaweza kusema ni kile kile ambacho macho ya undani wa mtu yameona na hawezi kukieleza kwa maneno ya ulimi wake. Anakiona rohoni mwake kwa bujiweka mahali pa Mtanzania msanii ili aweze kukiona hicho kitu. Labda tunaweza kusema ni utashi ambao Mtanzania, msanii aliouona miongoni mwa jamii yake na akatafsiri kwa njia ya rangi au gogo la mti. Uwezo huu wa tafsiri ya utashi huu wa njia ya sanaa ndio usanii wenyewe na kila msann anao wa peke yake Hakuna msani anayefanana na msann mwingine kwa madhumuni haya Msann mzuri wa namna hn hachon au hachongi au haumbi sanaa mbili zilizo sawa sawa, kila moja ni tofauti na nyingine


6. Mama na Boga


7. Mama akisali

Kuhusu utaalamu wa juu wa uthamini wa sanaa mafunzo yake ni magumu. Kwa upande wa mtazamaji asiyekuwa na mafunzo yoyote akitazama sanaa anasema anaipenda, au ni nzuri lakini hawezi kutoa sababu kwa nini anaipenda

Kwa kuwa sanaa ni vitu muhimu katika maishaya watu na wanaishi navyo wakati wote ni jambo la maana kama watu wangefundishwa uthamini wa sanaa hizo. Wakisha pewa mafunzo hayo wangependa sanaa zao zaidi Masomo ya uthamini yanaweza kuendeshwa huko huko vijijini ambako sanaa hutengenezwa, na ingefaa yaende pamoja na mafunzo ya usanaa.

error: Jisajili kupata uhuru zaidi !!